Nusu ya wananchi wa Saudia wanalalamikia ugumu wa maisha
Uchunguzi wa hivi karibuni kabisa wa maoni unaonesha kuwa, nusu ya wananchi wa Saudia Arabia wanalalamikia ugumu wa maisha na kupanda vibaya kwa bei za bidhaa. Kwa mujibu wa al Khalij al Jadid, uchunguzi huo wa maoni umefanywa na shirika moja la kibiashara la eneo hili baada ya kuombwa kufanya hivyo na taasisi ya Marekani…
Mshikamano kambi ya muqawama, ujumbe wa Hamas wakutana na Sayyid Nasrullah
Ujumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS umeonana na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon mjini Beirut, ukiwa ni ushahidi wa kuzidi kushikamana kambi ya muqawama katika eneo hili. Shirika la habari la Quds limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, ujumbe huo wa ngazi za juu wa HAMAS…
Azimio la Ukraine dhidi ya Russia katika Umoja wa Mataifa lapingwa na nchi nyingi
Rasimu ya azimio la Ukraine la kutaka Russia ilaaniwe katika Umoja wa Mataifa limegonga mwamba baada ya kupingwa na aghalabu ya nchi za dunia. Azimio hilo limeungwa mkono na nchi 58 pekee kati ya nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwa ni idadi ndogo sana ikilianganishwa na nchi ambazo ziliunga mkono Kiev mwezi…
Makamu wa Rais wa Iran: Marekani na Ulaya hazina njia nyingine ghairi ya kukubali JCPOA
Makamu wa Rais wa Iran anayehusika na masuala ya uchumi amesema, vikwazo na mashinikizo ndiyo silaha ya mwisho kabisa ya Marekani na Ulaya na akaeleza kwamba katika hali ya sasa wao hawana njia nyingine isipokuwa kuyakubali mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Mohsen Rezaee aliyasema hayo hapo jana alipohutubia kabla ya Sala ya Ijumaa ya mjini…
Rais wa Syria asisitiza ulazima wa kupambana na misingi ya kifikra ya ugaidi
Rais Bashar al Assad wa Syria amesisitiza ulazima wa kupambana na misingi ya kifikra ya ugaidi na akaeleza kwamba, kupambana na ugaidi hakutawezekana kwa kutumia nguvu za kijeshi pekee, kwa sababu idiolojia ya mitazamo ya kufurutu ada haitambui mipaka bali inajipanua na kuenea kwa kasi kutoka nchi moja hadi nyingine. Rais wa Syria ameyasema hayo…
Mashambulizi haramu ya Marekani nchini Syria, nembo ya ubeberu wa Washington
John Kriby, mratibu wa mahusiano ya kiistratijia ya baraza la usalama wa taifa la ikulu ya Marekani, White House amejaribu kuhalalalisha mashambulio haramu ya nchi yake huko Syria na kudai kuwa, eti Washington haina nia ya kuzidisha machafuko katika eneo hili. Vile vile amedai kuwa, lengo la mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani huko Syria…
Palestina yataka uanachama kamili wa Umoja wa Mataifa lakini Marekani inapinga
Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeanzisha tena msukumo wake wa kutaka uanachama kamili katika Umoja wa Mataifa (UN) huku Marekani ikiendeleza njama zake za muda mrefu za kupinga hatua hiyo. “Tunajadiliana kwa nia njema na wanachama wote Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,” amesema Riyad Mansour, balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa huku…
Tangazo la jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya mmoja wa viongozi wa Jihad ya Kiislamu ya Palestina
Mahakama ya utawala wa Kizayuni ilitoa mashtaka dhidi ya mmoja wa viongozi mashuhuri wa harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina na kumtuhumu kwa uchochezi dhidi ya utawala huo na ugaidi. Mahakama ya Ofar ya utawala wa Kizayuni ilitoa hati ya mashtaka dhidi ya Bassam Al-Saadi, mmoja wa viongozi mashuhuri wa Jihad ya Kiislamu, aliyetiwa…