Ubeberu wa kimataifa

Marekani inaiba 80% ya mafuta yanayozalishwa Syria kila siku

Marekani inaiba 80% ya mafuta yanayozalishwa Syria kila siku

Marekani inapora asilimia 80 ya mafuta yanayozalishwa kwa siku nchini Syria. Wizara ya Mafuta ya Syria imesema vikosi vamizi vya Marekani vinaiba mapipa 66,000 za mafuta ghafi kwa siku katika nchi hiyo ya Kiarabu. Kwa mujibu wa wizara hiyo, kiwango hicho kinachoibiwa na wanajeshi vamizi wa Marekani katika nch hiyo inayoshuhudia vita tangu mwaka 2011,…

HAMAS: Muqawama ndio njia bora kabisa ya kuikomboa ardhi ya Palestina

HAMAS: Muqawama ndio njia bora kabisa ya kuikomboa ardhi ya Palestina

Mjumbe mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, muqawama na mapambano ndio njia bora kabisa ya kuzikomboa ardhi za Palestina na kuifanya Palestina kuwa huru. Ismail Ridhwan amesisitiza kuwa, jibu la Wapalestina kwa jinai za utawala ghasibu wa Israel unaokalia Quds kwa mabavu litakuwa ni mtutu wa bunduki. Kiongozi huyo…

Israel yakiri kuwaua watoto Wapalestina Gaza

Israel yakiri kuwaua watoto Wapalestina Gaza

Utawala wa Kizayuni wa Israel umekiri kuwaua watoto watano Wapalestina katika hujuma yake ya hivi karibuni dhidi ya Ukanda wa Gaza. Utawala huo dhalimu ulianzisha  vita dhidi ya Gaza mnamo Agosti 5 na vita hivyo vilimalizika baada ya siku tatu kufuatia upatanishi wa Misri. Jumla ya watu 49 waliuawa shahidi katika hujuma hiyo ya Israel…

Austria ni kitovu cha chuki dhidi ya Uislamu Ulaya

Austria ni kitovu cha chuki dhidi ya Uislamu Ulaya

Austria ni maarufu kwa usanifu majengo mzuri na sanaa, hata hivyo, cha kusikitisha ni kwamba, nchi hii sasa imejijengea sifa nyingine katika miaka ya hivi karibuni: ile ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya Waislamu waliowachache. Kulingana na data iliyotolewa Juni 2022, zaidi ya matukio 1000 ya chuki dhidi ya Uislamu yaliripotiwa mwaka uliopita; ongezeko la…

Kukiri Mkuu wa Sera za Nje wa EU kwamba Magharibi imeonyesha undumakuwili katika kadhia za Ukraine na Gaza

Kukiri Mkuu wa Sera za Nje wa EU kwamba Magharibi imeonyesha undumakuwili katika kadhia za Ukraine na Gaza

Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amekiri kuwa nchi za Magharibi zinatumia vipimo vya nyuso mbili na za undumilakuwili kuhusiana na masuala ya kimataifa. Akijibu suali aliloulizwa katika moja ya mahojiano aliyofanyiwa, kuhusu msimamo wa Umoja wa Ulaya kwa watu wa Ukraine na Gaza; pamoja na Borrell kukiri kuwa vimetumika vipimo vya…

DAESH (ISIS) wametumia asilimia 90 ya silaha za Marekani katika operesheni za kigaidi

DAESH (ISIS) wametumia asilimia 90 ya silaha za Marekani katika operesheni za kigaidi

Mtaalamu mmoja wa masuala ya kiusalama amesema, asilimia 90 ya wahanga na waathirika wa ugaidi nchini Iraq hasa katika maeneo yaliyokombolewa wameuliwa kwa silaha za Marekani. Japokuwa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh limeshindwa na kusambaratishwa katika nchi za Iraq na Syria, mabaki ya magaidi wa kundi hilo yangaliko katika nchi hizo na Marekani…

Wanachama 13 wa genge la kigaidi la al Shabab waangamizwa Somalia

Wanachama 13 wa genge la kigaidi la al Shabab waangamizwa Somalia

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, wanachama 13 wa genge la kigaidi ukufurishaji la al Shabab wameangamizwa katika shambulio la anga lililofanywa katikati ya Somalia. Maafisa wa kijeshi wa Somalia wametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, shambulio la anga lililofanywa nchini humo dhidi ya maficho ya magaidi wa al Shabab katika mkoa wa Hiran limeua wanamgambo…

Iran: Muqawama wa Kiislamu hauishii tu katika ukanda wa Asia Magharibi

Iran: Muqawama wa Kiislamu hauishii tu katika ukanda wa Asia Magharibi

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, muqawama na mapambano ya Kiislamu si kitu cha kuishia kwenye eneo moja tu. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA,  Ali Bahadori Jahromi alisema hayo jana kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa mnasaba wa tarehe 23 Mordad kwa kalenda ya Kiirani ya…