Ubeberu wa kimataifa

Kani: Israel inakoseshwa usingizi na kizazi kipya cha Wapalestina

Kani: Israel inakoseshwa usingizi na kizazi kipya cha Wapalestina

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema kuwaua watoto wa Kipalestina kumegeuka na kuwa jambo la kawaida kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, na umwagaji damu huo unadhihirisha wazi kuwa Wazayuni wanakiogopa kizazi kipya cha Wapalestina. Ali Bagheri Kani alisema hayo jana hapa Tehran katika mazungumzo yake na Mohammed bin Abdulaziz al-Khulaifi,…

Magaidi 50 wa Daesh wahamishiwa Iraq kutoka nchini Syria

Magaidi 50 wa Daesh wahamishiwa Iraq kutoka nchini Syria

Kitengo cha upashaji habari cha jeshi la Iraq kimetoa ripoti rasmi na kusema kuwa karibu wanachama 50 wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Dashe (ISIS) wamehamishiwa mkoani Nainawa (Nineveh) Iraq kutoka katika kambi ya al Hawl ya nchini Syria. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hivi sasa kuna takriban wakazi 56,000 katika kambi ya…

Wamagharibi wakosolewa kwa undumakuwili juu ya vita Ukraine na Gaza

Wamagharibi wakosolewa kwa undumakuwili juu ya vita Ukraine na Gaza

Harakati inayopinga dhulma na ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina imekosoa vikali undumakuwili wa nchi za Magharibi kuhusu vita nchini Ukraine kwa upande mmoja na katika Ukanda wa Gaza, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa upande mwingine. Harakati ya Kimataifa ya Kuususia Utawala haramu wa Israel BDS katika taarifa jana Jumamosi…

Nyayo za mafia Waisraeli katika madai ya Wizara ya Sheria ya  Marekani dhidi ya IRGC

Nyayo za mafia Waisraeli katika madai ya Wizara ya Sheria ya Marekani dhidi ya IRGC

Wizara ya Sheria ya Marekani imechapisha taarifa inayodai kuwa mtu mmoja kwa jina Shahram Poursafi, ambaye wizara hiyo ilimtaja kuwa mwanachama wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), alipanga kumtumia Mmarekani mmoja kumuua John Bolton na afisa mwingine wa utawala wa Donald Trump. Madhumuni ya njama hiyo imetajwa kuwa ni kulipiza kisasi…

Ghalibaf: Muqawama wa Palestina umetoa bishara ya kuangamia utawala wa Kizayuni

Ghalibaf: Muqawama wa Palestina umetoa bishara ya kuangamia utawala wa Kizayuni

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, muqawama na mapambano ya harakati ya Jihad al Islami ya Palestina mbele ya utawala wa Kizayuni wa Israel yametoa bishara njema ya kuangamia utawala huo pandikizi. Shirika la habari la IRNA limemnkuu Mohammad Bagher Ghalibaf akisema hayo leo katika kikao cha wazi cha Bunge…

Wazayuni 10 walijeruhiwa kwa kupigwa risasi katika mji wa Jerusalem unaokaliwa kimabavu

Wazayuni 10 walijeruhiwa kwa kupigwa risasi katika mji wa Jerusalem unaokaliwa kimabavu

Polisi ya Kizayuni imetangaza kuwa, Wazayuni 10 walijeruhiwa katika shambulizi la asubuhi katika basi moja mjini Jerusalem inayokaliwa ki mabavu. Shirika la habari la Palestina la Shahab limeripoti kuwa wapiganaji wa makundi ya muqawama waliwafyatulia risasi Wazayuni waliokuwa kwenye kituo cha mabasi huko mjini Jerusalem. Kanali ya habari ya Elium ya Urusi imeripoti kuwa Wazayuni…

Russia yaonya juu ya uwezekano wa kuvunja uhusiano na Marekani

Russia yaonya juu ya uwezekano wa kuvunja uhusiano na Marekani

Afisa mmoja katika wizara ya mambo ya nje ya Russia ameonya kuwa uhusiano wa nchi hiyo na Marekani unaweza ukafika kwenye “nukta isiyoweza kurudishika nyuma” na mbaya zaidi kuliko ya hivi sasa. Alexander Darchiev, mkuu wa idara ya Amerika Kaskazini katika wizara ya mambo ya nje ya Russia amesema, ikiwa Seneti ya Marekai itapitisha mipango inayolenga…

Sisitizo la Kiongozi Muadhamu kuhusu kuinuliwa hadhi ya Harakati ya Jihad Islami

Sisitizo la Kiongozi Muadhamu kuhusu kuinuliwa hadhi ya Harakati ya Jihad Islami

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amejibu barua ya Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina na kusema, “mapambano (muqawama) ya kishujaa ya Jihad Islami yatapelekea kupanda hadhi ya harakati hiyo katika mapambano sambamba na kusambaratisha hadaa za utawala wa Kizayuni na kuufedhehesha utawala huo.” Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi…