Mwandishi murtadi aliyemtusi Mtume SAW yu mahututi kwenye mashine ya kupumulia
Msemaji wa Salman Rushdie, mwandishi murtadi wa kitabu cha Aya za Shetani kinachomtusi na kumvunjia heshima Bwana Mtume Muhammad SAW, na ambaye ameshambuiwa kwa kuchomwa kisu mjini New York Marekani, ametangaza kuwa, baada ya kufanyiwa upasuaji uliochukua saa kadhaa, hivi sasa Rushdie anasaidiwa kuvuta pumzi kwa mashine ya kupumulia, lakini hawezi kuongea. Kwa mujibu wa…
HAMAS yapongeza misimamo ya waziri wa ulinzi wa Pakistan dhidi ya Israel
Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amepongeza msimamo thabiti ulioonyeshwa na waziri wa ulinzi wa Pakistan dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel. Waziri wa ulinzi wa Pakistan Khawaja Muhammad Asef ameieleza serikali ya Uingereza na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo kuwa Azimio la Balfour la mwaka…
Qatar kujenga upya Ukanda wa Gaza
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas ilitangaza kuwa, nchi ya Qatar ilikubali kujenga upya nyumba zilizoharibiwa wakati wa mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza. Ismail Haniyeh, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina alitangaza Ijumaa mchana kuwa alikuwa na mazungumzo ya…
Athari za mashambulio ya Yemen zinaendelea, Wakuwait wakatazwa kutumia drone Imarati
Athari za mashambulio ya kulipiza kisasi na ya kujihami ya wananchi wa Yemen dhidi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) bado zingalipo na sasa serikali ya Kuwait imewataka wananchi wake wasitumie ndege yoyote isiyo na rubani wanapokuwa nchini Imarati, ili wasije wakajiingiza kwenye matatizo. Baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu kufanya jinai kubwa…
Juhudi za Marekani za kueneza ushawishi wake barani Afrika
Akiwa katika safari yake ya kuzitembelea nchi kadhaa za Afrika, Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, amezungumza na kushauriana na viongozi wa nchi alizozitembelea kuhusu masuala ya usalama, mgogoro wa chakula na jinsi ya kuzishirikisha nchi za Kiafrika katika vita vya Ukraine. Katika safari hiyo, ametembelea Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya…
Israel imewaua shahidi watoto Wapalestina zaidi ya 1,000 tangu 2008
Tangu mwaka 2008, zaidi ya watoto elfu moja wa Kipalestina wameuawa shahidi katika Ukanda wa Gaza katika mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya Al-Mayadeen siku ya Alkhamisi, mashahidi 15 kati ya 43 wa mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza…
Jibu la Kiongozi Muadhamu kwa Barua ya Katibu Mkuu wa Jihad Islami ya Palestina
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amejibu barua ya Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina na kusema, “mapambano (muqawama) ya kishujaa ya Jihad Islami yatapelekea kupanda hadhi ya harakati hii katika mapambano sambamba na kusambaratisha hadaa za utawala wa Kizayuni na kuufedhehesha utawala huo.” Kwa mujibu wa taarifa ya tovuti ya Ofisi…
Katibu MKuu wa UN apongeza amani katika uchaguzi wa Kenya
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wananchi wa Kenya kwa kupiga kura kwa amani wakati wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika hapo juzi Agosti 9, 2022 Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu Stéphane Dujarric kutoka New York Marekani imesema Katibu Mkuu anatambua kazi muhimu iliyofanywa na mamlaka ya Kenya pamoja…