Mjukuu wa Mandela: Mapinduzi ya Kiislamu yameipa ilhamu Afrika Kusini
Mjukuu wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amesema Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanatoa ilhamu na motisha kwa taifa hilo la kusini mwa Afrika. Mandla Mandela ambaye yuko Tehran kwa ajili ya kupokea Tuzo ya Haki za Binadamu za Kiislamu amesema hayo katika mazungumzo yake na Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya…
Onyo la Katibu Mkuu wa UN la kutokea vita vya nyuklia duniani
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya kuhusu hatari ya kutokea vita vya nyuklia duniani. Alitoa onyo hilo Jumatatu, Agosti 1, 2022 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kuangaliwa Upya Mkataba wa NPT wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia. Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New…
Wazayuni wavamia msikiti wa al Aqsa na kuwatia nguvuni Wapalestina 12
Jeshi la utawala haramu wa Israel limewatia nguvu Wapalestina 12 sambamba na kundi la walowezi wa Kizayuni kuuhujumu msikiti mtukufu wa al Aqsa, ambacho ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu. Msikiti wa al Aqsa ambao ni nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu-Kipalestina katika mji wa Baitul Muqaddas umekuwa ukilengwa na hujuma na hatua za uharibifu za…
Kufutwa siku ya mapumziko (maombolezo) ya Ashura katika kalenda rasmi ya Afghanistan
Kwa mujibu wa ripoti zilizochapishwa, Taliban imeondoa likizo au siku ya maombolezo ya Ashura katika kalenda rasmi ya Afghanistan na badala yake kuweka mahala pake matukio kadhaa yanayohusiana nayo. Hii ni katika hali ambayo kabla ya hapo siku hii ya Ashura ilikuwa imesajiliwa katika kalenda rasmi ya Afghanistan kama siku ya mapumziko ya umma kwa…
Kuwait: Tutaendelea kuisusia Israeli na makampuni yanayoshirikiana nayo
Kuwait imetangaza kuwa itaendelea kuisusia Israel, bidhaa zake na makampuni yanayoshirikiana nayo. Hayo yametangazwa katika Mkutano wa Maafisa wa Ofisi za Kikanda za Kuisusia Israel. Shirika la Habari la Kuwait (KUNA) lilimnukuu mwakilishi wa Kuwait katika mkutano huo, Mashari Al-Jarallah, akisema, “Bidhaa zote ambazo zinashukiwa kuwa za Israeli au za kampuni zilizopigwa marufuku, zinachukuliwa hatua…
Mauaji ya Ayman al Zawahiri yapokewa kwa hisia tofauti
Mauaji ya Ayman al Zawahiri, kiongozi wa mtandao wa al Qaida katika operesheni ya droni iliyofanywa na wanajeshi wa Marekani, yamepokewa kwa hisia tofauti ya duru za kisiasa za nchi hiyo. Mapema leo asubuhi, rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza habari ya kuuawa Ayman al Zawahiri katika shambulio la ndege isiyo na rubani lililofanywa na…
Makumi ya viongozi wa serikali ya Saudia watiwa mbaroni kwa kula rushwa
Serikali ya Saudi Arabia imewatia mbaroni maafisa 78 wa serikali kwa tuhuma za ufisadi, kula rushwa, utapeli, kutakatisha fedha na kutumia vibaya madaraka yao. Taasisi ya kupambana na ufisadi nchini Saudi Arabia, kwa miaka kadhaa sasa imekuwa ikichunguza kesi nyingi za ubadhirifu na ufisaidi na hadi hivi sasa mamia ya wafanyakazi wa hivi sasa na…
Sheikh Naim Qassem: Israel haina budi kutambua rasmi haki za maliasili za Lebanon
Naibu Katibu MKuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel hauna budi kuzitambua rasmi haki za Lebanon zinazohusiana na utajiri wa maliasili za baharini. Sheikh Naim Qassem ameyasema hayo katika majlisi kuu ya Ashura na kusisitiza kuwa, Wamarekani inawapasa waache kushirikiana na Wazayuni katika kutafuta na kuchimba gesi katika eneo la…