Iraq yakaribisha taarifa ya Baraza la Usalama la UN dhidi ya mashambulio ya Uturuki
Wizara ya mambo ya nje ya Iraq imeonyesha msimamo wake wa kwanza kuhusiana na taarifa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kutangaza kuwa, matini ya taarifa hiyo inaunga mkono misimamo ya nchi hiyo. Jumatano iliyopita, Uturuki ilishambulia mji wa kitalii wa Zakho ulioko kwenye mkoa wa Dahok nchini Iraq na kuua watu…
Magendo ya binadamu yameongezeka mara 26 katika mpaka hatari zaidi duniani
Wizara ya usalama wa ndani ya Marekani imetangaza kuwa, pato linalopatikana katika biashara haramu ya magendo ya binadamu inayofanywa kupitia mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Mexico, ambao ni mpaka hatari zaidi duniani, limeongezeka kutoka dola milioni 500 mwaka 2018 na kufikia dola bilioni 13 kwa sasa. Tovuti ya gazeti la New York Times…
Waislamu wa Tanzania waadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds na kulaani jina za Israel
Upendo na na hisia ya Waislamu wa Tanzania kwa Palestina huonekana katika mambo kadhaa moja wapo ni hili hapa. Waislamu nchini Tanzania na wapenda amani katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki leo wameungana na wapigania haki duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni…
Jenerali Hajizadeh: Karibuni hivi roketi la kubebea satalaiti la Qaem litakuwa tayari kutumwa angani
Kamanda wa kikosi cha anga za mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema roketi la kubebea satalaiti la Qaem karibuni hivi litakuwa tayari kurushwa kwa ajili ya kutumwa katika anga za mbali. Katika miaka miwili iliyopita, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imejikita katika uundaji maroketi ya kubebea satalaiti na kuweza kupiga hatua…
Baada ya kutimuliwa Russia, shirika la uhajiri wa Mayahudi kuhamishiwa Israel
Sambamba na kushadidi mivutano katika uhusiano wa Russia na Israel, duru za habari zimeripoti kuwa shirika la uhajiri wa Mayahudi limeandaa mpango wa siri wa kuhamishia Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) ofisi yake iliyokuweko mjini Moscow. Gazeti la Jerusalem Post limezinukuu duru za kuaminika zikiripoti kuwa kufuatia uamuzi wa Russia wa kuifunga ofisi ya shirika la…
UN yapitisha azimio dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel
Umoja wa Mataifa umepitisha azimio linalosisitiza kuwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel hauna haki ya kupora rasilimali za watu wa Palestina na za miinuko ya Golan ya Syria unayoikalia kwa mabavu. Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC) limepitisha rasimu ya azimio iliyowasilishwa kwa ushirikiano wa Pakistan,- kwa niaba ya kundi…
Trump azikosoa Sera za Biden dhidi ya Iran
Rais huyo wa zamani wa Marekani alikosoa sera za utawala wa Biden dhidi ya Iran. Rais mstaafu wa Marekani, Bw. Donald Trump, amekuwa akimkosoa Rais Joe Biden hivi majuzi huku akizikosoa sera zake kuhusu Iran kulingana na taarifa za hivi punde. Kwa mujibu wa ripoti ya Newsmax, Trump alidai katika hotuba yake kwamba serikali ya…
Wapalestina 21 wauawa, kujeruhiwa na askari wa Israel Ukingo wa Magharibi
Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limewaua shahidi Wapalestina wawili na kujeruhi wengine 19 katika miji ya Nablus na Jenin katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu. Kwa mujibu wa shirika la habari la Ma’an la Palestina, Wapalestina hao wameuawa na kujeruhiwa mapema leo baada ya wanajeshi makatili wa…