Nasrallah: Hizbullah ilikataa hongo ya Marekani kusitisha makabiliano na Israel
Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon anasema harakati hiyo ilikataa mapendekezo kadhaa ya hongo ya kifedha ya Marekani ili kusitisha mapambano yake na utawala wa Kizayuni wa Israel . Katika mahojiano ya aina yake yaliyorekodiwa miaka 20 iliyopita na kurushwa hewani wiki hii, Katibu Mkuu wa Hezbollah Sayyed Nasrallah anasema harakati hiyo ya mapambano…
Mfalme wa Bahrain amuuzulu waziri wake kwa kukataa kumpa mkono balozi wa Israel
Mfalme wa Bahrain amemuuzulu waziri mwanamke wa nchi hiyo kwa kukataa kumpa mkono balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa mjini Manama na kwa kupinga hatua ya kuanzisha ya uhusiano wa kawaida na utawala huo haramu. Tovuti ya habari ya Shahab News imeripoti kuwa, hivi karibuni ilifanyika hafla katika makazi ya balozi wa Marekani…
Wanamuqawama wa Iraq wataka jibu kwa shambulio la Uturuki
Harakati ya Muqawama ya Asa’ib Ahl al-Haq ya Iraq imelitaka Bunge la nchi hiyo lichukue hatua za kivitendo kujibu mashambulizi ya anga ya Uturuki katika eneo la Kurdistan, lililoua na kujeruhi makumi ya raia. Katika taarifa, kundi hilo la muqawama nchini Iraq limeihutubu Uturuki kwa kusema: Uvamizi, kuendelea kukiuka mamlaka ya kujitawala Iraq, kukalia kwa…
Jeshi la Syria latungua makombora ya Israel viungani mwa Damascus
Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Syria kimetangaza kutungua makombora yaliyokuwa yamevurumishwa na utawala haramu wa Israel nje ya mji mkuu Damascus. Shirika rasmi la habari la Syria, SANA limetangaza kuwa, mizinga ya ulinzi wa anga ya Syria alfajiri ya leo Ijumaa imetungua akthari ya makombora hayo ya Israel viungani mwa Damascus. Jeshi katili…
Wabunge Ufaransa walaani sera za apathaidi za Israel
dadi kubwa ya wabunge katika Bunge la Kitaifa la Ufaransa wametia saini rasimu ya azimio la kulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na sera zake za ubaguzi wa rangi au apatahidi na jinai za kivita dhidi ya Wapalestina. Azimio hilo ambalo lina kichwa kisemacho: “Kutaasisishwa Utawa wa Apathaidi Dhidi ya Watu wa Palestina” limeidhinishwa…
Tanzania yapinga hatua ya Marekani kutambua Quds kama mji mkuu wa Israel
Tanzania imetangaza rasmi kupinga uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani kutambua mji wa Quds (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Akizungumza na gazeti la The Citizen, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Augustino Mahiga amesema Tanzania kama ilivyo kwa jamii yote ya kimataifa haitambui Jerusalem…
Ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wenye asili ya Asia umekithiri Marekani
Matokeo ya utafiti uliofanywa katika majimbo mbalimbali ya Marekani yanaonyesha kuwa, vitendo na mienendo ya ubaguzi wa rangi dhidi ya raia wa nchi hiyo wenye asili ya Asia imeongezeka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Kwa mujibu wa gazeti la The Guardian, matokeo ya utafiti uliofanywa katika majimbo tofauti ya Marekani na kituo cha binafsi…
Kuridhishwa kwa Iran na matokeo ya mkutano wa Tehran, Harakati dhidi ya Umagharibi yazidi kuimarika
Ziara ya hivi karibuni ya marais wa Uturuki na Russia mjini Tehran na kukutana na wakuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo iliakisiwa pakubwa na vyombo vya habari vya dunia, kwa mujibu wa wachunguzi na wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa, ni muungano mpya dhidi ya serikali ya Iran. Magharibi. Gazeti la Lebanon la…