Balozi wa Palestina aitaka jumuiya ya kimataifa kuilaani Israel
Haya ni maneno ya Balozi wa Palestina nchini Tanzania akiitaka Jumuiya ya kimataifa ilaani vitendo vya utawala haramu wa Israel kama inavyolaani vitendo vya Russia huko Ukraine, Dar es Salaam. Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hamdi Mansour Abuali ameitaka jumuiya ya kimataifa kulaani vitendo vya Israel kukiuka makubaliano na Palestina kama ambavyo wamekuwa wakilaani uvamizi wa…
Iran: Israel ndio mzizi wa ugaidi na ukosefu wa usalama Asia Magharibi
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ndio chimbuko la vitendo vya kigaidi na ukosefu wa usalama na uthabiti katika eneo hili la Asia Magharibi. Naser Kan’ani alisema hayo jana Jumanne na kuongeza kuwa, hatua ya Marekani kuukingia kifua na kuunga mkono utawala…
Maseneta waitaka serikali ya Biden kuwajibika kuhusu uchunguzi wa mauaji ya Shireen
Maseneta wa chama cha Democratic cha Marekani wameitaka serikali ya Rais Joe Biden wa nchi hiyo kuwajibika kuhusu uchunguzi unaohusu mauaji ya mwandishi wa habari wa Palestina wa televisheni ya Al Jazeera, Shireen Abu Akleh. Ni baada ya Umoja wa Mataifa kumesema kuwa taarifa ulizokusanya zinaonesha kuwa, Shireen Abu Akleh, mwandishi wa habari wa televisheni ya…
MAREKANI, TANZANIA KIWAKILISHI CHA ‘DUNIA’ MBILI KATI YA TATU ZINAZOKIDHANA KUHUSU ISRAEL
Uchambuzi wa Kisiasa kuhusu Uhusiano wa Tanzania na Israel. MAPEMA wiki iliyopita na wiki hii dunia imeshuhudia historia ikiwekwa kwa husiano za kidiplomasia linapokuja Taifa la Israel baada ya Tanzania na Marekani kwa nyakati hizo mbili tofauti kufungua balozi mpya katika Taifa hilo la Mashariki ya Kati. Wakati Tanzania ikifungua ubalozi mara ya kwanza nchini…
China yapinga vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya mauzo ya mafuta ya Iran
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ameeleza kuwa, ushirikiano kati ya Beijing na Tehran uko ndani ya fremu ya sheria za kimataifa na kutangaza upinzani wake dhidi ya vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Iran. Siku ya Alhamisi, tarehe 16 Julai/Julai 6, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China alitoa…
Waziri Mkuu Uingereza ajiuzulu
London. Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amejiuzulu nafasi ya kiongozi wa Chama cha Conservative. Boris amejiuzulu nafasi hiyo leo Alhamisi Julai 7, 2022 lakini bado atabaki kuwa Waziri Mkuu mapaka chama hicho kitakapopata kiongozi mpya mwezi Oktoba. Katika hotuba yake, Boris amesema “Nina huzuni kuacha kazi bora zaidi duniani. Ninataka ujue jinsi ninavyohuzunishwa na kuacha…
Russia yaharibu mifumo ya makombora ya Marekani nchini Ukraine
Jeshi la Russia limetangaza habari ya kusambaratisha mifumo miwili ya makombora aina ya HIMARS ya Marekani mashariki mwa Ukraine. Wizara ya Ulinzi wa Russia imesema vikosi vya nchi hiyo jana Jumatano vilifanikiwa kuharibu mifumo hiyo miwili ya makombora ya kisasa karibu na medani ya vita katika kijiji kimoja kilichoko katika mji wa Kramatorsk, eneo la Donetsk. Igor…
Waziri wa Utamaduni wa Yemen: Mamluki wa Saudia wanaiba athari za kale za Yemen
Waziri wa Utamaduni wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen ametangaza kwamba mamluki wa Saudi Arabia na washirika wake wanajaribu kupora athari za kale za nchi hiyo. Abdullah Ahmad al-Kibsi, Waziri wa Utamaduni wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen, amesema mamluki wa muungano vamizi unaoongozwa na Saudia wanafanya juhudi za kuiba vitu na…