
Marekani yatangaza vikwazo vipya dhidi ya sekta ya mafuta ya Iran
Wizara ya Fedha ya Marekani imeendeleza uraibu wa nchi hiyo wa kuziwekea vikwazo nchi mbalimbali kwa kutangaza vikwazo vipya dhidi ya sekta ya mafuta na petrokemikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Wizara ya Hazina ya Marekani jana Jumatano ilitangaza kuziwekea vikwazo kampuni mbalimbali zenye makao yao katika Umoja wa Falme za Kiarabu, eti kwa kufanikisha…

Marekani yafumbia macho ukweli kuhusu mauaji ya Shireen Abu Akleh
Licha ya kuwepo ushahidi na dalili za wazi kuhusu mauaji ya Shireen Abu Akleh, mwandishi ya televisheni ya al-Jazeera ya nchini Qata, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetoa taarifa ikidai kwamba mauaji hayo hayakuwa ya makusudi. Hii ni katika hali ambayo mauaji hayo yalitekelezwa mbele ya macho ya mamilioni ya walimwengu na bila…

Russia: Mashambulio ya anga ya Israel dhidi ya Syria hayakubaliki hata kidogo
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imelaani vikali shambulio la anga lililofanywa hivi karibuni na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Syria. Siku ya Jumamosi, ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zilishambulia kitongoji cha Hamidiyah kusini mwa mkoa wa Tartus. Raia wawili walijeruhiwa katika shambulio hilo. Katika taarifa, wizara…

Familia ya Shireen yakosoa ripoti ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani
Watu wa familia ya Shireen Abu Akleh, mwandishi habari Mpalestina ambaye aliuliwa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel akiripoti matukio yaliyokuwa yakijiri katika mji wa Jenin, wamokosoa vikali ripoti iliyotolewa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani kuhusu mauaji hayo. Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani imetangaza…

Maandamano Marekani baada ya polisi kumuua kijana Mwafrika-Mmarekani
Maelfu ya waandamanaji waliokuwa na hasira waliingia barabarani katika jimbo la Ohio, katikati mwa Marekani siku ya Jumapili kulaani kitendo cha polisi kumuua kikatili kijana mwenye asili ya Kiafrika ambaye hakuwa na silaha. Maandamano hayo yameitishwa baada ya kusambaa klipu za video zinazoonyesha uhalifu huo wa kishetani. Klipu hizo za kuogofya zilionyesha maafisa wanane wa…

Raisi: Historia haitasahau kamwe uhalifu wa Marekani dhidi ya taifa la Vietnam
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika hafla ya kupokea hati za utambulisho za balozi mpya wa Vietnam mjini Tehran kwamba historia haitasahau kamwe jinai zilizofanywa na Marekani dhidi ya taifa la Vietnam. Inakadiriwa kuwa, zaidi ya milioni tatu waliuawa wakati wa vita vya Marekani dhidi ya taifa la Vietnam. Vilevile karibu galoni milioni 18 na…

Mshauri wa Rais wa Iran: Magaidi wa ISIS wametokana na fikra za Kimarekani
Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kaumu na waliowachache kidini amesema kundi la kigaidi la ISIS au Daesh limetokana na fikra za Kimarekani. Kwa mujibu wa taarifa ya IRNA, Mamusta Abdulsalam Karimi Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kaumu na waliowachache kidini aliyasema…

Uturuki yaikamata meli ya mizigo ya Urusi
Balozi wa Ukraine mjini Ankara alidai kuwa Uturuki ilikamata meli ya mizigo ya Urusi iliyokuwa imebeba nafaka za Ukraine. Shirika la habari la Reuters lilimnukuu balozi wa Ukraine mjini Ankara akisema kuwa forodha ya Uturuki imekamata meli ya mizigo ya Urusi iliyobeba nafaka za Ukraine. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu aliahidi…