Ubeberu wa kimataifa

Takwimu za hivi punde kuhusu uhalifu na jinai za muungano wa Saudia dhidi ya Yemen

Takwimu za hivi punde kuhusu uhalifu na jinai za muungano wa Saudia dhidi ya Yemen

Katika takwimu zake za hivi punde kuhusu jinai za muungano wa Saudia nchini Yemen, shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la Intisaf limeripoti kuwa zaidi ya wanawake na watoto 6,000 waliuawa kishahidi na zaidi ya 6,000 walijeruhiwa. Kwa mujibu wa Idhaa ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Fars, shirika la kulinda haki…

Russia yaishutumu Marekani kwa kukwamisha Mazungumzo ya Ukraine

Russia yaishutumu Marekani kwa kukwamisha Mazungumzo ya Ukraine

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergeĭ Viktorovich Lavrov ameishutumu vikali Marekani kwa siasa zake kuhusu vita vya Ukraine na kusema kuwa, Washington ndiyo inayokwamisha kufikiwa makubaliano baina ya Moscow na Kyiv hata katika masuala madogo kabisa. Amesema, hivi sasa Marekani inawatwisha viongozi wa Ukraine misimamo yake na ndio maana Kyiv inakwamisha kila kitu…

Medvedev: Urusi yawaweka maadui zake sehemu wanayostahiki, miongoni mwao Marekani

Medvedev: Urusi yawaweka maadui zake sehemu wanayostahiki, miongoni mwao Marekani

Naibu Katibu wa Baraza la Usalama la Russia amesema kuwa Marekani imezusha hofu ya kuchukiza nchini Urusi katika jaribio la kuipigia magoti Moscow na kuisambaratisha. Alisema kuwa Urusi ina uwezo wa kuwaweka maadui wake wote wabaya mahali pake. Kwa mujibu wa Idhaa ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Fars, Dmitry Medvedev alisema siku ya…

Moncef Marzouki amelaani kitendo cha jinai huku akiwaonya viongozi wa Saudia kwa kuua umati wa watu

Moncef Marzouki amelaani kitendo cha jinai huku akiwaonya viongozi wa Saudia kwa kuua umati wa watu

Rais wa zamani wa Tunisia amewaonya viongozi wa Saudi Arabia kwa hatua yao ya kutekeleza adhabu ya kifo kwa watu 81 kwa siku moja na kuwaambia wajiandae kwa madhara ya hatua yao hiyo. Siku ya Jumamosi, wizara ya mambo ya ndani ya Saudia iitekeleza adhabu ya kifo kwa watu 81 ikidai kuwa watu hao wamefanya…

Saudi Arabia yawanyonga watu 81 ndani ya siku moja, watu 7 kati ya walionyongwa ni Wayemeni

Saudi Arabia yawanyonga watu 81 ndani ya siku moja, watu 7 kati ya walionyongwa ni Wayemeni

Kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari, Saudi Arabia iliwanyonga watu 81 katika siku moja kwa uhalifu unaohusiana na “ugaidi”, Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia imethibitisha mkasa huo wa hukumu za kifo za watu 81 na kutangaza kuwa imetekeleza hukumu hiyo kwa watu hao. Shirika la habari la AFP…

Iran ni nchi ya kwanza ya Kiislamu kurusha satalaiti kwenye anga za mbali

Iran ni nchi ya kwanza ya Kiislamu kurusha satalaiti kwenye anga za mbali

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema kuwa na uwezo wa kujirushia satalaiti katika anga za mbali ni kigezo cha nchi iliyostawi duniani na kuongeza kuwa, pamoja na kuwepo vikwazo vingi vya kimataifa, vijana wa taifa la Iran katika IRGC wamefanikiwa kurusha satalaiti katika anga za mbali. Jana Jeshi la Walinzi…

Iran ; Utawala wa Kizayuni utarajie Jibu Kali kwa Jinai walioitenda

Iran ; Utawala wa Kizayuni utarajie Jibu Kali kwa Jinai walioitenda

Ndege za kivita za Israel zilishambulia eneo la Reef mjini Damascus – Syria mnamo siku ya Jumatatu asubuhi (Machi 6), na kuwaua Wairani wawili miongoni mwa watetezi wa Haram tukufu. Wawili hao wakifahamika kama Morteza Saeed Nejad na Ehsan Karbalaeipour waliuawa huku Tehran ikisisitiza kuwa, italipiza kisasi cha damu za mashahidi wake, na kuhusiana na…

Imarati Yajenga vitongoji kwa ajili ya askari wa Israel katika mji wa Socotra, Yemen

Imarati Yajenga vitongoji kwa ajili ya askari wa Israel katika mji wa Socotra, Yemen

Umoja wa Falme za Kiarabu umeripotiwa kujenga vitongoji katika kisiwa cha kistratijia cha Yemen cha Socotra ambacho kinakaliwa kwa mabavu na Imarati, kwa ajili wanajeshi wa utawala haramu wa Israel; zaidi ya mwaka mmoja baada ya tawala hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kawaida. Tovuti ya habari ya “Yemen News Portal” imenukuu vyanzo vya habari ambavyo…