
Chad yatangaza siku 3 za maombolezo baada ya kuuawa makumi ya wanajeshi
Serikali ya Chad imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa baada ya kuuawa makumi ya wanajeshi wake katika jimbo la Lac. Serikali ya Chad imetangaza kuwa kuanzia leo usiku hadi siku ya Ijumaa bendera zote nchini humo zitapepea nusu mlingoti na hafla na sherehe zote haziruhusiwi kufanyika katika siku za maombolezo. Vyombo vya habari na…

Algeria: UNRWA inapaswa kufanya kazi hadi kuundwa kwa taifa la Palestina
Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria ilisema kwamba kupigwa marufuku shughuli za UNRWA katika ardhi za Palestina inayokaliwa kwa mabavu kuna madhara makubwa na mabaya sana kwa mamilioni ya wakazi wake. Wizara hiyo imesema katika taarifa yake: “Tunalaani vikali kuidhinishwa kwa sheria mbili za utawala wa Kizayuni kwa lengo la kudhoofisha shughuli za UNRWA…

Reuters: BRICS kujadili mpango mpya wa kimataifa wa mabadilishano ya fedha
Russia itawasilisha pendekezo lake la mfumo mpya wa fedha wa kimataifa kwa mataifa mengine wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya BRICS katika mkutano wa kilele wa kundi hilo utakaofanyika wiki ijayo nchini humo. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Reuters likinukuu waraka uliosambazwa na Moscow kwa waandishi wa habari kabla…

Sisitizo la Joe Biden la kudumisha uwepo wa kijeshi wa Marekani Asia Magharibi
White House ilitangaza siku ya Jumanne kwamba, Rais Joe Biden wa Marekani ameiandikia barua Congress ya nchi hiyo akiifahamisha kwamba vikosi vya Marekani vitaendelea kubakia katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) kwa kuhofia jibu la Iran kwa chokochoko za utawala wa Kizayuni. Akizungumzia jibu la makombora la Tehran kwa mashambulizi ya Israel, Rais…

Hamas yathibitisha rasmi kuuawa kwa Yahya al-Sinwar
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilithibitisha rasmi kuuawa shahidi Yahya Sanwar, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya harakati hio. “Khalil al-Hayya”, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas katika Ukanda wa Gaza, mchana wa leo (Ijumaa), katika ujumbe uliotangazwa kwenye mtandao wa “Al-Aqsa”, alithibitisha rasmi kuuawa shahidi “Yahya Al-Sinwar” , aliyekua mkuu…

Tanzania inaunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa la kutaka Israel ijiondoe kutoka katika ukanda wa Gaza
Tanzania imepiga kura kuunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa linaloitaka Israel kukomesha uwepo wake wa “kinyume cha sheria” katika Ukanda wa Gaza. Azimio hilo lililopitishwa, linaitaka Israel kujiondoa katika Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki ndani ya mwaka mmoja huku mzozo na Hamas ukikaribia kuadhimisha mwaka wake wa kwanza mnamo tarehe 7, mwezi Oktoba….

Jeshi la Uganda limetishia kumfukuza balozi wa Marekani nchini humo
Kufuatia vikwazo vya hivi karibuni vya Washington dhidi ya maafisa wanne wa polisi wa nchi hiyo, kamanda wa jeshi la Uganda alimuonya balozi wa Marekani kwamba anapaswa kuondoka katika nchi hio ya Afrika Mashariki ikiwa hatamuomba radhi rais wa Uganda. Muhozi Kainerugaba, Mkuu wa Majeshi ya Uganda, alimuonya Balozi wa Marekani nchini kwamba ikiwa hatamuomba…

Waziri Mkuu wa Burkina Faso: Ukraine inalenga kukuza ugaidi Barani Afrika kwa nia ya kuidhoofisha Russia
Waziri Mkuu wa Burkina Faso, Apollinaire Kyelem de Tambela amesema, Ukraine inayasaidia makundi ya magaidi katika eneo la Sahel barani Afrika; na inafanya hivyo kwa nia ya kuidhoofisha Russia ambayo inashirikiana kijeshi na nchi za eneo hilo. Tambela ambaye yuko nchini Russia anakohudhuria kongamano la Siku za Kiuchumi za Burkina Faso, ameeleza hayo katika mahojiano na…