Israel iliomba kukataliwa kwa malalamiko mapya ya Afrika Kusini katika Mahakama ya The Hague
Tel Aviv iliiomba Mahakama ya Hague kukataa ombi jipya la #Afrika_Kusini la kutoa amri ya dharura kuhusu operesheni ya jeshi la #Israeli huko #Rafah. Katika nyaraka zilizochapishwa hivi majuzi na Mahakama ya Kimataifa ya Haki, Israel imesema kuwa hukumu ya awali iliyotolewa na mahakama hii inajumuisha “hali ya jumla ya uhasama huko Gaza” na kwa…
Rais Tshisekedi: Niko tayari kusitisha mpango wa kuanzisha vita na Rwanda
Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema kuwa, yuko tayari kusitisha mpango wake wa kuanzisha vita na jirani yake Rwanda, ili kutoa nafasi kwa jitihada zinazoendelea za kupata suluhu ya mzozo unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo. Matamshi yake yamekuja siku chache baada ya Marekani, Ufaransa na washirika wao, kuitaka Rwanda iache kuwasaidia…
Ripoti ya kulengwa kwa meli iliyopo kaskazini mwa Djibouti
Vyanzo vya habari vya Uingereza vilisema kwamba meli ya kibiashara ililengwa na ndege isiyo na rubani katika maji katika masafa ya kilomita 110 kaskazini mwa Djibouti. Siku ya Jumanne asubuhi, vyanzo vya ndani viliripoti tukio la usalama kwa meli katika eneo la mlango bahari la “Bab Al-Mandab”. Shirika la Usafiri wa Majini la Uingereza limesema…
Sheikh Zakzaky: Adui amewaua Wapalestina 20,000 dhidi ya wapiganaji 4,000.
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ameeleza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni chimbuko la wahyi kwa mataifa ya Kiislamu dhidi ya madhalimu wenye kiburi, na kuhusu vita vya Ghaza amesema kua: wakati idadi ya wapiganaji wa Hamas ni 4,000 tu, adui ameua zaidi ya Wapalestina 20,000 hadi sasa, na Wengi wao katika…
Je, Afrika Mashariki ina msimamo gani kuhusu vita vya Israel na Hamas? Mtaalam anafunua maoni ya Kenya, Tanzania, na Uganda.
Katika picha: Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu walitia saini makubaliano mjini Jerusalem mwaka 2016. Mwitikio wa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kwa mzozo unaoendelea huko Gaza umekuwa mdogo kuliko wa Afrika Kusini. Bunge la Afrika Kusini limepitisha azimio la kufunga ubalozi wake mjini Tel Aviv….
Congo DR yaiomba jamii ya kimataifa kuiwekea vikwazo Rwanda ili iache ‘kuwaunga mkono waasi wa M23’
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeiomba jamii ya kimataifa kuiwekea vikwazo nchi jirani ya Rwanda ikiituhumu kuwasaidia waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo. Akizungumza na vyombo vya habari, msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Patrick Muyaya, amesema kuwa kamwe hatajadiliana na kundi la M23, ingawa kundi hilo limesisitiza kuwa liko tayari…
Umoja wa Afrika wazuia ujumbe wa Israel kuingia katika makao yake makuu
Chanzo cha kidiplomasia cha Afrika kimeiambia televisheni ya Al Jazeera ya Qatar kwamba Umoja wa Afrika umewazuia wajumbe wa utawala ghasibu wa Israel kuingia katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, ambao walikuwa wameomba kukutana na maafisa wa Afrika kwa madhumuni ya kuwasilisha maoni ya serikali ya Tel Aviv kuhusu vita vinavyoendelea huko…
Wanawake nchini Kenya wafanya sherehe ya giza katika siku ya wapendanao
Mamia ya wanawake wa Kenya wafanya sherehe ya giza ya wapendanao kukomesha mauaji ya wanawake nchini. Huku watu ulimwenguni wakisherehekea Siku ya Wapendanao kwa maua na chokoleti, wanawake wa Kenya wakiwa katika maombolezo wakiwa wamevalia nguo nyeusi na kuwasha mishumaa na kushikilia waridi jekundu katika hafla ya kuwaenzi wanawake zaidi ya 30 waliouawa nchini humo…