Tel Aviv inasubiri kilichoandaliwa na Marekani kwa ajili ya maelewano ya kikanda
Waziri wa vita wa Israel Bani Gantz amesema Israel na mataifa ya Ghuba ya Kiarabu, Misri na Jordan yanatarajiwa kufanya kazi pamoja sio tu katika kukabiliana na Iran, bali wanapaswa kuunda nguvu ya kikanda inayoongozwa na Marekani ili kuimarisha nguvu za pande zote zinazohusika, na jitihada zinafanywa kupanua ushirikiano huu. Akielezea wakati wa kuimarishwa kwa nguvu…
Kiongozi Muadhamu: Sera za Iran zinatoa kipaumbele juu ya kuimarisha uhusiano na majirani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kipaumbele katika sera za kigeni za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi sasa ni kuimarisha uhusiano na mataifa jirani. Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hayo leo katika mazungumzo yake na Rais Serdar Berdimuhamedow wa Turkmenistan na kuongeza kuwa: Kuimarisha uhusiano wa pande mbili na…
Wajackoyah Kuimarisha Biashara Ya Bangi
Faraan; Ingawa mwaniaji kiti cha Urais kwa tikiti ya chama chake cha Roots Party Prof George Wajackoyah ni mgeni katika siasa za humu nchini, amejizolea umaarufu kwa kutoa ahadi zake kwamba atahalalisha matumizi na uuzaji wa bangi au marijuana. Prof Wajackoya anasema mauzo ya bhangi ndio suluhu ya matatizo ya kiuchumi yanayokumba nchi hii. Prof…
Yemen yaahidi kushambulia vituo vya mafuta vya Saudia endapo itaendelea kuiba mafuta yao
Ofisa wa ngazi ya juu wa Yemen ameonya kuwa, vikosi vya jeshi la Yemen vitashambulia vituo vya mafuta ndani kabisa ya Saudi Arabia, iwapo muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Riyadh utaendelea kupora mafuta wa Wayemen. Mohammad Tahir Anam, mshauri wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema vikosi vya Yemen havitakaa kimya na kuruhusu…
Sakaja Adai Ana Digrii
Faraan ; Seneta Johnson Sakaja anayepingwa kuwania ugavana wa Nairobi kwa madai hana Digirii, Jumatatu alisema alisoma katika Chuo Kikuu cha Teams University na kuhitimu Oktoba 2016. Katika ushahidi aliowasilisha kwa jopo la Tume ya Uchaguzi (IEBC) la kutatua mizozo ya uteuzi na uidhinishaji wa wawaniaji, Bw Sakaja anayedaiwa hajahitimu kwa shahada hiyo, alidai wamepotoka…
Mfumuko wa bei wafikia asilimia 3.7
Dodoma ; Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema katika mwaka 2021 mfumuko wa bei uliongezeka kwa wastani wa asillimia 3.7 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.3 mwaka 2020. Dk Mwigulu amesema hayo leo Jumanne Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha hali ya uchumi wa Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa…
Jenerali wa Kizayuni akiri: Israel haitashinda katika vita vijavyo
Jenerali mmoja wa jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ameashiria udhaifu wa jeshi la utawala huo na kusisitiza kuwa, endapo hali hiyo haitabadilika, Israel haitashinda katika vita vijavyo. Kwa mujibu wa chaneli ya 14 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni, Yitzhak Barik, jenerali mkongwe katika jeshi la utawala haramu wa Israel na mkuu wa…
Ugiriki yaachilia huru meli ya mafuta ya Iran baada ya kukiuka amri ya Marekani
Serikali ya Ugiriki imebatilisha uamuzi wake wa hivi karibuni wa kuteka meli moja ya mafuta ya Iran na hivyo kukaidi mashinikizo ya Marekani ambayo ndiyo iliyoamuru meli hiyo ikamatwe. Kwa mujibu wa taarifa ya Jumanne ya Shirika la Bandari na Usafiri wa Baharini la Iran, serikali ya Ugiriki imeamuru meli hiyo iachiliwe pamoja na mzigo…