
Iran na Oman zatiliana saini hati 12 za kustawisha ushirikiano + Video
Leo Jumatatu, Rais Ebrahim Raisi amefanya ziara rasmi ya siku moja nchini Oman na kupokewa kwa heshima zote na Sultan Haitham bin Tariq wa nchi hiyo. Miongoni mwa matunda ya ziara hiyo rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Oman ni kutiwa saini hati 12 za kustawisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi…

Vyanzo vya habari Syria: Katika uchaguzi nchini Lebanon, msimamo wa washirika wa Syria uliimarishwa
Moja kati ya duru za ngazi ya juu nchini Syria imesisitiza kuwa, washirika wa nchi hiyo wakiongozwa na harakati ya Hizbullah waliweza kuunganisha misimamo yao katika uchaguzi wa Lebanon. Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Habari la Fars News, chanzo kikuu cha Syria kilisema kuwa kulingana na sheria ya uchaguzi ya Lebanon, takwimu hizo…

Umoja wa Mataifa wasikitishwa na hatua ya Mali ya kujitoa katika kikosi cha kupambana na ugaidi
Umoja wa Mataifa umesikitishwa na uamuzi wa nchi ya Mali ya kujiondoa katika kikosi cha kundi la nchi tano za eneo la Sahel linalojulikana kama G5 ambalo lilibuniwa mwaka 2014 kwa ajili ya kupambana na ugaidi katika eneo hilo. Bi Martha Pobee, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya siasa barani Afrika…

Kiongozi wa Korea Kaskazini naye pia vilevile hamtaki Biden
Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani, Jake Sullivan alisema Washington haikuona dalili yoyote ya Korea Kaskazini kutaka kufanya mkutano wa pande mbili kati ya kiongozi wa Marekani Kim Jong Un na Rais wa Marekani Joe Biden. Sullivan anasafiri hadi Asia Mashariki na Rais wa Marekani Joe Biden, alipoulizwa kwenye ndege ikiwa Pyongyang inataka mkutano…

Saudia: Tuna hamu ya kuzungumza na Iran kuhusu kisima cha gesi cha Arash
Waziri wa Nishati wa Saudi Arabia amesema kuwa nchi yake na Kuwait zina hamu ya kuzungumza na Iran kuhusu kisima cha gesi cha Arash au al Durra. Kuwait na Saudi Arabia tarehe 21 Machi mwaka huu zilisaini hati kwa ajili ya kuendeleza kisima cha gesi cha Arash; ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Kampuni ya…

Hassan Sheikh Mahmoud ateuliwa kuwa rais mpya wa Somalia
Bunge na seneti ya Somalia zimemchagua rais wa zamani Bw. Hassan Sheikh Mahmoud kuwa rais wa nchi hiyo kwa muhula wa miaka minne. Vyanzo vya habari viliripoti ushindi wa Rais wa zamani wa Somalia Hassan Sheikh Mahmoud uliopatikana kupitia uchaguzi wa bunge na kufanikiwa kua raisi kwa muhula wa miaka minne. Alikuwa rais wa nane…

Raila amtaja Martha Karua kuwa mgombea mwenza: ‘inawezekana’
Mgombea urais wa Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga hatimaye amemteuwa kiongozi wa Narc-Kenya Martha Karua kuwa mgombea mwenza. Akimtaja kwenye hafla iliyofanyika Jumatatu Raila alisema kwamba Jopo la Azimio la Kuteuwa Mgombea Mwenza lilitoa ripoti na kusema Karua aliibuka bora kwa nafasi hiyo. Jopo hilo pia lilikuwa limewahoji magavana Charity Ngilu…

Sadr abadilika kuwa mpinzani wa taifa
Kiongozi wa mrengo wa Sadr nchini Irak amesema hajafaulu kuunda serikali ya kitaifa ya walio wengi na kuongeza kuwa kuna njia moja pekee iliyosalia nayo ni upinzani wa kitaifa. Muqtada al-Sadr aliandika katika tweet yake: “Nilipewa heshima kubwa kuwa na muungano mkubwa na maarufu zaidi wa bunge katika historia ya Iraq.”Nilipata heshima ya kuunda kizuizi…