
Mwisho wa upigaji kura katika uchaguzi wa Lebanon
Muda wa kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Lebanon umekwisha na shughuli za kuhesabu kura nchini humo kuanza. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars News, muda wa upigaji kura ulipokamilika nchini Lebanon, vituo sita vya kupigia kura vilifungwa nchini humo na shughuli za kuhesabu kura katika uchaguzi wa bunge zilianza. Al-Jazeera imeinukuu…

Mohammed bin Zayed ateuliwa kuwa rais wa Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati)
Baraza Kuu la Muungano wa Falme za Kiarabu limemteua Mohammed bin Zayed Aal Nahyan kuwa rais mpya wa nchi hiyo. Televisheni ya al Jazeera imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, uteuzi huo umekuja baada ya kufariki dunia rais wa nchi hiyo, Sheikh Khalifa bin Zayed Aal Nahyan. Khalifa bin Zayed alifariki dunia jana Ijumaa akiwa…

Sonko, Nassir Kukutana Ana Kwa Ana Hafla Ya Azimio Tononoka
ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko, ameapa kuhudhuria mkutano wa hadhara unaotarajiwa kuongozwa na kinara wa ODM, Bw Raila Odinga, katika uwanja wa Tononoka ulio Mombasa kesho Jumamosi. Iwapo mkutano huo utafanyika ilivyopangwa, itakuwa ni mara ya kwanza Bw Sonko kukutana hadharani na Mbunge wa Mvita, Bw Abdulswamad Nassir, ambao wote ni wagombeaji ugavana…

Kina Mdee wasubiri hukumu
Baada ya kazi ya kuthibitisha barua za kukata rufaa kupinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya Chadema, wabunge hao wa viti maalumu sasa wameitwa ukumbini kusikiliza hukumu yao. Mchakato wa kuwahoji wabunge hao 19 wa viti maalumu ulianza rasmi katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam ambapo Baraza Kuu la Chadema linaendelea likiwa na…

Moscow: Pfizer na Moderna walihusika katika mpango wa kijeshi wa kibaolojia nchini Ukraine
Afisa wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi alisema kuwa rais wa sasa wa Marekani amesimamia binafsi uendeshaji wa maabara za kibaolojia nchini Ukraine, akiongeza kuwa makampuni ya dawa ya Pfizer na Moderna pia yalihusika katika mpango huo. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Fars, licha ya jitihada za Marekani na washirika wake…

Kauli zenye kulaani kuuawa kishahidi mwandishi wa habari wa Al-Jazeera wa Kipalestina na wanamgambo wa Kizayuni.
Pande mbalimbali zimesisitiza ulazima wa ufufunguzi wa mashtaka dhidi ya utawala wa Kizayuni kwa mauaji ya mwandishi wa habari wa Al-Jazeera. Shirin Nasri Abu Aqleh mwandishi habari Mpalestina wa Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar ameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel alipokuwa akiakisi machafuko katika kambi ya wakimbizi Wapalestina mjini Jenin. Kwa mujibu…

Samia aeleza mkakati kupunguza makali ongezeko bei ya mafuta
Dar es Salaam; Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza mkakati wa kubana matumizi ya Serikali katika bajeti ya matumizi ili kupata fedha za kupunguza makali ya ongezeko la bei ya mafuta linalosababisha kuongezeka kwa bei za bidhaa na huduma nchini. Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu Mei 9, 2022 katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari…

Jordan: Masjidul-Aqswa ni mali ya Waislamu, Israel yatakiwa kutoitahini subira ya Waislamu bilioni 2
Kamati ya Palestina katika Bunge la Jordan imesisitiza kuwa, Waislamu wana mamlaka mutlaki kwa msikiti mtakatifu wa al-Aqswa ulioko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Kamati hiyo imeuonya utawala ghasibu wa Israel na kuutaka usiitahini subira ya Waislamu bilioni 2 ulimwenguni. Msimamo huo wa Kamati ya Palestina katika Bunge la Jordan umetolewa kufuatia matamshi ya Naftali Bennett, Waziri…