
Ukosefu wa usawa wa kijinsia Katika Muungano Wa Ruto
NAIBU RAIS William Ruto jana alitia saini mkataba wa ushirikiano na vyama 12 chini ya Muungano wa Kenya Kwanza huku viongozi wa muungano huo ukiendeshwa na midume tupu. Vyama vyote vinavyounga azima yake vinasimamiwa na wanaume ishara kwamba, maamuzi yote ya muungano wa Kenya Kwanza huenda yatakuwa yakifanywa na jinsia moja.Japo alisifu washirika wake akisema…

Putin: Marekani inapandisha bei ya nishati duniani
Rais wa Urusi ailaumu Marekani kwa kupanda kwa bei ya nishati duniani, akisema nchi zisizo rafiki hazitimizi makubaliano yao na Moscow. Kulingana na Huduma ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Fars.Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumatano alisema kuwa Marekani ndiyo ya kulaumiwa kwa kupanda kwa bei ya nishati ulimwenguni. “Nchi zisizo rafiki…

Nasrullah: Watu wa Palestina hawatashindwa katika mapambano yao dhidi ya Wazayuni
Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, wananchi wa Palestina hawatashindwa katika mapambano yao ya ukombozi dhidi ya utawala ghasibu wa Israel. Akizungumzia matukio ya sasa ya Lebanon na eneo la Magharibi mwa Asia Jumatatu jioni, Katibu Mkuu wa Hizbullah aliwaambia Wazayuni kuwa: “Ikiwa mnadhani kwamba Wapalestina watakata takaa na…

Ukandamizaji wa Al-Khalifa; Kukamatwa na kuteswa kwa ndugu watatu matineja wa Bahrain
Mohammed, Muqtada na Montazer Al-Kuwaiti ni ndugu watatu kutoka nchi ya Bahrain, wenye umri baina ya miaka 14 na 15, ambao walihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani na Al Khalifa mwaka 2021 kwa mashtaka ya uwongo pamoja na mateso na vitisho. Wameshtakiwa kwa kushiriki katika maandamano, utengenezaji wa vifaa vinavyoweza kushika au kusababisha moto, kusababisha…

Ruto aenda kinyume na NCIC, Atoa Wimbo Wa ‘Sipangwingwi’
NAIBU wa Rais, William Ruto amekaidi amri ya Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa (NCIC) baada ya kutoa wimbo ambao ameupa jina ‘Hatupangwingwi’, muda wa saa chache baada ya tume hiyo kulipiga marufuku neno hilo. Siku ya Ijumaa saa tano mchana, Tume ya NCIC iliorodhesha neno hilo kuwa miongoni mwa maneno 23 ambayo yanafaa…

Hassan Joho afifia kisiasa
USHAWISHI wa Gavana wa Mombasa, Bw Hassan Joho, kwa siasa za Pwani na kitaifa kwa jumla umekosekana kwa takriban wiki mbili sasa baada ya kuugua kwake. Ilibainika Bw Joho alianza kuugua punde alipowasili nchini kutoka ziara ya Uingereza ambapo alikuwa ameandamana pamoja na Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na wanasiasa wengine wa Muungano wa…

Amerika, EU Wawinda Mabinti Wa Rais Putin
AMERIKA na Muungano wa Mataifa ya Ulaya (EU) sasa zinalenga mabinti wa kiongozi wa Urusi Vladimir Putin katika juhudi za kumshinikiza kuondoa majeshi yake nchini Ukraine. Kulingana na ripoti zilizochapishwa Jumatano katika majarida ya Wall Street Journal na Bloomberg, Amerika na EU zinalenga kuwekea vikwazo vya kiuchumi mabinti hao; Maria Vorontsova na Katerina Tikhonova kufuatia hatua ya baba yao,…

NATO: Vita vya Ukraine vinaweza kuchukua miezi kadhaa au miaka
Katibu Mkuu wa NATO atangaza uwezekano wa kurefushwa kwa vita kati ya Urusi na Ukraine na hitaji la kuimarisha na kudumisha utayari wa muungano. Kwa mujibu wa Huduma ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Fars, Katibu Mkuu wa NATO alionya Jumatano usiku kwamba vita vya Ukraine vinaweza kudumu kwa miezi au hata miaka na…