
Safari za ndege kutoka Uwanja wa Ndege wa Sanaa hadi Cairo zaanza upya
Mkurugenzi mkuu wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sanaa alitangaza kwamba safari za ndege kuelekea Cairo, ambayo ilikuwa imezingirwa na Saudi Arabia, zitaanza tena hivi karibuni. Khalid al-Shaif, mkurugenzi mkuu wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sanaa, alitangaza siku ya Jumatatu kwamba safari za ndege kutoka uwanja wa ndege hadi Cairo zitaanza tena…

Wanajeshi wa Israel wawashambilia waumini wa Kipalestina huko al-Quds, Ramadhani 2
Vikosi vya utawala wa Israel vimewashambulia Wapalestina katika Lango la Damascus huko al-Quds inayokaliwa kwa mabavu na kuwapiga vikali waumini wa Kipalestina na kuwatia mbaroni wengine katika usiku wa pili wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ni jambo la kawaida kwa vikosi vya Israel kuzidisha ghasia dhidi ya Wapalestina wanaokusanyika katika eneo hilo wakati wa mfungo…

Utawala wa Kizayuni hauwezi kamwe kuliondoa doa la hatia usoni mwake
Amiri Jeshi Mkuu wa Kundi Maarufu La Ukombozi wa Palestina Alitangaza kwamba mauaji ya wapiganaji watatu wa muqawama yaliyotekelezwa na adui wa Kizayuni, Kamwe hayawezi kutengeneza sura ya utawala huu ambao umetiwa doa na risasi za upinzani. Kundi hilo lilitoa taarifa kua: Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kumbukumbu ya Siku ya Dunia na kwa mujibu…

Hotuba ya Sayyid Hassan Nasrallah kwa mnasaba wa Mwezi wa Ramadhani
Kwa mujibu wa taarifa, hotuba hiyo itarushwa mubashara au moja kwa moja kupitia televisheni ya Al Manar saa mbili na nusu usiku kwa wakati wa Beirut na Afrika Mashariki. Sayyid Hassan Nasrallah atazungumza kuhusu masuala mbali mbali katika hotuba hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na wengi.

Tel Aviv ilituma wajumbe wa usalama mjini Cairo kwa hofu ya maandamano
Duru za Misri zimefichua kuwa, utawala wa Kizayuni ulituma ujumbe wa usalama mjini Cairo kwa hofu ya kutokea mlipuko kwa mnasaba wa matukio yajayo ya Palestina. Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Fars News Agency, duru za Misri zimesema kuwa, ujumbe wa usalama wa Kizayuni hivi karibuni ulisafiri hadi Cairo na kukutana na maafisa…

Maandamano nchini Italia kuhusu mauzo ya silaha kwa serikali iliyojiuzulu ya Yemen
Waandamanaji wa Italia walikusanyika katika mji wa bandari wa Genoa kuzuia upakiaji wa silaha zitakazotumwa kwa serikali ya Yemen iliyojiuzulu. Raia wa mji wa Genoa nchini Italia walifanya maandamano siku ya Ijumaa asubuhi kupinga utumaji wa silaha kwa serikali ya Yemen iliyojiuzulu. Wananchi wa Genoa, wakiwemo wanafunzi na wanachama wa vyama vya wafanyakazi, waliandamana hadi…

Dar es Salaam; Mangula ang’atuka, Kinana kumrithi
Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) imempendekeza Katibu mkuu wa zamani wa chama hicho, Abdulrahman Kinana kuwa mgombea nafasi ya makamu mwenyekiti (Bara) baada ya aliyekuwa akishika nafasi hiyo, Philip Mangula kung’atuka. Hayo yamesemwa leo Alhamis Machi 31, 2022 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza na waandishi wa…

Washirika Wa Uhuru Wamkwepa Raila
MASWALI yameibuka kuhusu hali ya kampeni za Azimio La Umoja huku washirika wa Rais Uhuru Kenyatta hasa kutoka eneo la Mlima Kenya na mashariki mwa nchi wakionekana kulegeza kamba katika juhudi za kumpigia debe mgombeaji urais wa muungano huo, Raila Odinga. Hii ni baada ya wanasiasa wa chama cha Jubilee na washirika wake kutoonekana katika…