Uchambuzi wa Kisiasa

Waziri wa Ulinzi wa Russia: Vikosi vya nyuklia vilianza shughli zake kulingana na amri ya Putin

Waziri wa Ulinzi wa Russia: Vikosi vya nyuklia vilianza shughli zake kulingana na amri ya Putin

Waziri wa Ulinzi wa Russia alitangaza kuanza kwa majukumu ya vikosi vya kimkakati vya nchi hiyo kufuatia amri ya Rais Vladimir Putin wa Russia. Kulingana na vyanzo vya habari, Waziri wa Ulinzi wa Urusi alitangaza alasiri ya Jumatatu tarehe 28/2/2022 kwa majira ya Tehran: “Kwa kufuatia agizo la Rais, nyadhifa za Kamanda wa Kikosi cha…

Ubabe wa Marekani wafikia ukingoni

Ubabe wa Marekani wafikia ukingoni

Mkuu wa sera za kigeni katika Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina (Hamas) amesema moja kati ya mafunzo yanayopatikana katika vita vya Russia na Ukraine ni kuwa, zama za ubabe wa Marekani duniani zimefika ukingoni. Moussa Abu Marzouk mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas na ambaye pia ni mkuu wa sera za kigeni katika harakati hiyo…

Mazungumzo ya Russia na Ukraine mjini Belarus hayajulikani hatima yake

Mazungumzo ya Russia na Ukraine mjini Belarus hayajulikani hatima yake

Televisheni ya taifa ya Russia imetangaza kuwa duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya wajumbe wa nchi hiyo na Ukraine imemalizika nchini Belarus, lakini haijafahamika iwapo mazungumzo hayo yataendelea au la. Mazungumzo yana lengo la kuzima moto wa vita vilivyoanza Alkhamisi iliyopita kati ya nchi hizo mbili. Awali mkuu wa timu ya mazungumzo ya Russia huko…

Chama cha upinzani Morocco chalaani pupa ya serikali ya nchi hiyo ya kupatana na Wazayuni

Chama cha upinzani Morocco chalaani pupa ya serikali ya nchi hiyo ya kupatana na Wazayuni

Chama cha upinzani cha “al Adala wa al Tanmiya” cha Morocco kimelaani ziara ya waziri wa uchumi na viwanda wa utawala wa Kizayuni nchini humo. Chama hicho kimetoa taarifa rasmi na kusema kuwa kinalaani kwa nguvu zote ziara ya waziri wa uchumi na viwanda wa utawala wa Kizayuni mjini Rabat na pupa ya Morocco ya…

Jeshi la Yemen laitungua droni ya pili ya Marekani katika mkoa wa Ma’rib

Jeshi la Yemen laitungua droni ya pili ya Marekani katika mkoa wa Ma’rib

Jeshi la Yemen likishirikiana na vikosi vya kujitolea vya wananchi zimeitungua ndege ya pili isiyo na rubani iliyoundwa na Marekani. Katika miezi kadhaa iliyopita, jeshi la Yemen limefanikiwa kuzitungua droni kadhaa za muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia zilizokuwa zikitekeleza operesheni za hujuma katika maeneo mbalimbali ya ardhi ya Yemen. Msemaji wa vikosi…

Usambazaji wa silaha 10,000 na maagizo ya uhamasishaji wa raia

Usambazaji wa silaha 10,000 na maagizo ya uhamasishaji wa raia

Maafisa wa Ukraine wanasambaza bunduki kwa raia, na mapigano makali yanaendelea katika baadhi ya miji ya mpakani. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Fars ; Takriban ndani ya masaa 18 baada ya kuanza kwa operesheni maalum ya kijeshi ya Urusi katika eneo la Denbas, maafisa wa Ukraine walisambaza bunduki kwa raia, na…

Sayyid Hashem Safieddine: Ukraine ilifanya makosa kuitegemea Marekani

Sayyid Hashem Safieddine: Ukraine ilifanya makosa kuitegemea Marekani

Mkuu wa Baraza Kuu la harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema ni makosa kwa baadhi ya nchi kutegemea uungwaji mkono na himaya ya Marekani, na kwamba kadhia ya Ukraine imethibitisha tena ukweli huo. Akizungumzia vita vya Ukraine, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Hizbullah, Sayyid Hashem Safieddine amesema kuwa Lebanon itajiondoa katika majanga yote kwa ukombozi wa…

Umoja wa Afrika waamuru kusitishwa kwa mgogoro wa Ukraine

Umoja wa Afrika waamuru kusitishwa kwa mgogoro wa Ukraine

Umoja wa Afrika umetoa mwito wa kusimamishwa haraka iwezekanavyo mgogoro wa Ukraine. Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, ambaye pia ni Rais wa Senegal Macky Sall, pamoja na Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Moussa Faki Mahamat wametangaza kusikitishwa kwao na vita baina ya Russia na Ukraine huko mashariki mwa Ulaya. Taarifa ya viongozi hao iliyotolewa na…