
Kongamano la kumuenzi Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Mohandes lafanyika Tunisia
Kundi la vyama vya siasa na asasi za kiraia nchini Tunisia zimefanya kongamano kwa mnasaba wa mwaka wa pili wa kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha’abi….

Kuondoka kwa Marekani kutoka kwenye eneo, ni moja kati ya matokeo ya kuuawa shahidi Soleimani
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema kufungasha virago na kuondoka vikosi vya jeshi la Marekani katika eneo la Asia Magharibi ni sehemu ndogo ya matokeo ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Katika taarifa jana Ijumaa, wizara hiyo imesema…

Idadi ya wanajeshi watoro yaongezeka katika jeshi la Israeli
Miongoni mwa habari za Israel zimeripoti kuwa idadi ya askari wanaotoroka jeshi la utawala huo inaongezeka kadri siku zinavyokwenda. Tovuti ya lugha ya Kiebrania ya “Walla” imeripoti kuwa, mwaka huu wa 2021 pekee idadi ya askari wa Isael wanaozungumza lugha y Kiarabu waliotoroka kutokana na kubaguliwa na vilevile wanajeshi wa kawaida wanaotoroka huduma za…

Iran Yalaani Mashambulizi ya Israel dhidi ya Latakia ya Syria
TEHRAN (FNA)- Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesikitishwa na mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya maghala ya chakula na dawa huko Latakia ya Syria, na kuutaja utawala wa Kizayuni kuwa chanzo cha ukosefu wa utulivu katika eneo hilo. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Saeed Khatibzadeh mnamo Jumatano…

Baqeri Kani: Hatua kadhaa katika suala la uondoaji vikwazo
Ali Bagheri Kani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa Iran katika mazungumzo ya nyuklia ya JCPOA amesema; kutokana na mazungumzo ya karibuni mjini Vienna, zimepigwa hatua nzuri katika suala la uondoaji vikwazo. Bw. Kani katika mazungumzo ya Vienna amesema kuwa; katika kipindi…

Kuondolewa vikwazo Iran; siri ya mafanikio ya mazungumzo ya Vienna
Mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 4+1 linaloundwa na mataifa ya Russia, China, Uingereza, Ufaransa pamoja Ujerumani yaliendelea tena leo huko Vienna Austria maudhui kuu ikiwa ni suala la kuondolewa vikwazo na kutilia mkazo mapendekezo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu masuala mawili muhimu, yaani uhakika kwamba vikwazo vimeondolewa na dhamana yake….

Rais wa Somalia amfuta kazi Waziri Mkuu wake, mzozo wapamba moto
Rais wa Somalia amemfuta kazi Waziri Mkuu wake wakati huu wa kuendelea uchaguzi wa bunge na hivyo kuzusha mzozo mpya wa kisiasa katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. Vyombo vya habari vimeripoti habari hiyo na kusema kuwa, Rais Mohamed Abdullahi Farmaajo alichukua hatua hiyo jana Jumapili akimtuhumu Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble kuwa anahusika…

Rais wa Lebanon Aoun atoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ‘ya dharura’ ya kitaifa
Beirut, Lebanon – Rais wa Lebanon Michel Aoun ametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya “haraka” ya kitaifa kati ya vyama tawala vya nchi hiyo huku akilaani miezi kadhaa ya kupooza kisiasa serikalini. “Uvurugaji wa kimakusudi, wa kimfumo na usio na msingi unaosababisha kuvunjika kwa taasisi na serikali lazima ukome,” Aoun alisema katika hotuba ya…