Safari ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani nchini Israel; Ni kwa ajili ya Kuunga mkono au ni onyo?
Waziri wa ulinzi wa Marekani alikutana na Waziri mwenzake na waziri mkuu wa Israel, na ingawa wahusika walijaribu kuficha tofauti zilizokuwepo, ila maneno yao yalidhihirisha vyema kuhusu hali mbaya ya Israel. Kidokezo cha uchambuzi. “Operesheni huko Gaza ni operesheni ya Israeli na siko hapa kuamuru kikomo cha muda wa kusitisha vita.” Haya ni maneno ya…
Obama naye pia apatwa na wasiwasi kuhusu kushindwa kwa Biden
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ana wasiwasi kwamba Biden atapoteza kiti chake cha uongozi katika marudiano katika raundi ya pili dhidi ya Trump katika uchaguzi wa mwaka 2024 huku kukiwa na umaarufu mdogo wa rais huyo wa Marekani kutokana na umri mkubwa alionao, jambo ambalo limeleta rabsha nyingi katika wapiga kura nchini Marekani….
Mvutano waongezeka huku uchaguzi ukikaribia Congo DR
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inajiandaa kwa ajili ya uchaguzi Jumatano ambao ima utaimarisha demokrasia yake au kuzua ghasia mpya huku mivutano ya kisiasa ikiongezeka na kutishia amani na usalama wa nchi hiyo. Takriban wapiga kura milioni 44 waliojiandikisha wanatazamiwa kupiga kura mnamo Desemba 20 katika taifa hilo kubwa la Afrika ya kati lenye takriban watu…
Hofu ya kupoteza muonekano yamfanya Raisi Biden kumkabili Netanyahu
Wakati wakuripoti “mvutano usio wakawaida” kati ya Tel Aviv na Washington, vyombo vya habari vya Kiebrania na Amerika vilitangaza shinikizo la Ikulu ya White House kwa Waziri Benjamin Netanyahu “kumaliza vita vya ardhini mjini Gaza” na kuelezea kua inaweza ikapelekea “kupoteza sifa na muonekano Raisi Biden”. “Mvutano usio na kifani unaendelea kati ya maafisa wa…
Biden: Israel inapoteza uungwaji mkono wa kimataifa / Netanyahu anapaswa kubadilisha baraza la mawaziri
Rais Joe Biden wa Marekani alikiri kuwa utawala wa Israel unapoteza uungaji mkono wa jumuiya ya kimataifa kutokana na mashambulizi ya kiholela na yaliyoenea katika Ukanda wa Gaza na mauaji ya maelfu ya raia wa Palestina. Rais wa Marekani Joe Biden aliuambia umati wa wafuasi wa chama cha Democratic mjini Washington siku ya Jumanne kwamba…
Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS yaitambua rasmi serikali ya Niger
Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imeitambua rasmi serikali mpya ya Niger ikiwa ni katika kulegeza misimamo yake ya kisiasa na kiuchumi kuhusiana na nchi hiyo. Omar Alieu Touray Mkuu wa Tume ya ECOWAS, amesema katika mkutano wa jumuiya hiyo huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria kwamba timu ya wakuu wa nchi…
Jamhuri 2023: Mudavadi Akaribisha Wageni Ikulu Ya Rais Badala Ya Gachagua
ITIFAKI za urais (presidency) wakati wa maadhimisho ya Jamhuri Dei 2023 zilionekana kukiukwa kutokana na jinsi viongozi wakuu serikalini walivyoondoka Bustani ya Uhuru, Nairobi. Kama ilivyo desturi, baada ya kiongozi wa nchi kuhutubu, huondoka rasmi kisha anafuatwa na mkewe – mama wa taifa, halafu naibu wake. Rais William Ruto alipohitimisha hotuba yake kwa taifa, alifuatwa…
Kenya yaadhimisha miaka 60 ya Uhuru
Taifa la Kenya leo linaadhimisha miaka 60 ya kujitawala baada ya miongo kadhaa ya mapambano yaliyopelekea kujinyakulia uhuru na kutimuliwa mkoloni Muingereza nchini humo mnamo mwaka 1963. Idadi ya watu wa Kenya wakati wa Uhuru ilikuwa milioni 8.6 tu. Leo, idadi ya watu inakadiriwa kuwa karibu milioni 53. Miaka 60 tangu kupata uhuru, Kenya sio…