Mahakama: Ni kinyume cha sheria kwa UK kuwapeleka Rwanda watafuta hifadhi
Mahakama ya Juu ya Uingereza imesema mpango wa serikali ya London wa kuwapeleka nchini Rwanda wakimbizi na waomba hifadhi walioko nchini humo unakiuka sheria. Mahakama hiyo imetoa uamuzi huo leo Jumatano ikisisitiza kuwa, mpango huo unawaweka katika hali hatarishi wakimbizi hao, hasa kwa kuzingatia kuwa baadhi yao waliikimbia nchi yao ya Rwanda na kuwarejesha huko…
Rais wa Liberia na mpinzani wake Boakai wakutana tena katika duru ya pili ya urais
Wananchi wa Liberia wanapiga kura leo Jumanne katika duru ya pili ya uchaguzi kati ya Rais George Weah na Makamu wa Rais wa zamani Joseph Boakai baada ya mchuano mkali wa duru ya kwanza ambapo hakuna aliyeweza kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura. Mwanasoka mashuhuri George Weah, 57, aliongoza kwenye duru ya kwanza ya…
Uchambuzi wa hisia za kufedhehesha za Imarati kwa jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza
Katika utafiti uliochapishwa na Kituo cha Mafunzo ya Mashariki ya Kati huko Washington (MEI), imeelezwa kuwa Imarati imekuwa na nafasi ya uungaji mkono mkubwa wa kieneo wa utawala huu katika kipindi chote cha shambulio la jinai la Israel dhidi ya Gaza – ambalo liliingia katika mkondo wa pili. Katika utafiti huu, imeelezwa kuwa vita ambavyo…
Siku ya 40 baada ya operesheni ya kimbunga cha Al-Aqsa / idadi ya mashahidi kupitia uvamizi wa utawala wa Kizayuni nchini Palestina yafikia elfu 11 / askari wa utawala wa Kizayuni wawasili katika hospitali ya al-Shifa huko Ghaza.
Jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina, K.M.V mashambulizi katika maeneo ya makazi, na vilevile hospitali bado zinaendelea katika siku ya 40 baada ya operesheni ya kimbunga cha Al-Aqsa, kiasi kwamba wanajeshi wa Kizayuni wakiwa chini ya wingu kubwa la mashambulizi ya anga waliingia katika hospitali ya al-Shifa iliyoko Ghaza baada ya siku…
Hotuba ya Ijumaa – Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi (Mkuu wa shule Jamia Urwatul Wuthqa – Lahore) Imetolewa katika msikiti wa: Masjid Baitul ul Ateeq Lahore – Pakistan November 10, 2023 Khutba ya 1: Dajjal wawili: Mmoja ni yule anayesema kua Hamas ni Mfuasi wa Ahlul-bayt, na mwingine anasema kua Hamas hamwamini Imam Ali (a) Taqwa ni…
Balozi wa Tel Aviv mjini Washington: Hatuwaui Raia wa kawaida
Licha ya kwamba raia zaidi ya elfu kumi na moja wameuwawa kishahidi katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza, balozi wa utawala huo mjini Washington anasema kuwa, mashambulizi ya Israel yanalengwa mno! Michelle Herzog, balozi wa Tel Aviv mjini Washington, anasema utawala huo unatafuta mpango wa muda mrefu wa Gaza na unashauriana na Marekani…
Vyombo vya habari vya Israel: Hadi kufikia sasa Nasrullah bado hajatumia kadi zake zote
Katika mkesha wa hotuba mpya ya Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, vyombo vya habari vya Israel viliendelea kuichambua hotuba ya Sayid Hassan Nasrallah wiki 2 zilizopita na kusisitiza kuwa bado hajatumia kadi zake zote na uwezo wa makombora wa muqawama wa Lebanon ni upo juu zaidi ya mawazo ya Tel Aviv. Katibu Mkuu wa…
Trump aunga mkono kuendelea kwa mashambulizi dhidi ya Gaza
Licha ya kuongezeka kwa wasiwasi kuhusu vifo vya raia mjini Gaza, rais huyo wa zamani wa Marekani alisema ni lazima vita viendelee. Licha ya kuongezeka kwa wasiwasi kuhusu vifo vya raia huko Gaza, Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alisema katika mahojiano mapya kwamba vita kati ya Israel na Hamas lazima viendelee. “Kwa hivyo…