Atakayemkabidhisha askari wa Ukraine aliyeivunjia heshima Qur’ani kuzawadiwa $168,000
Rais Madan Kadyrov, wa eneo la Russia linalojiendeshea mambo yake la Chechnya ametenga zawadi ya ruble milioni 10 za Kirusi ambazo ni sawa na dola 168,000 za Kimarekani kwa atakayefanikisha kukamatwa akiwa hai, askari wa jeshi la Ukraine aliyeivunjia heshima Qur’ani tukufu kwa kuichoma moto nakala ya kitabu hicho kitakatifu. Tovuti ya kituo cha habari…
Ujumbe muhimu zaidi wa mazoezi ya pamoja kati ya Iran, Urusi na China
Amir Admiral Shahram Irani, kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza ulazima wa kudhaminiwa usalama katika eneo kwa kusisitiza kuwa, nchi za eneo hili ni katika vyanzo vikubwa zaidi vya mafuta duniani. Amiri wa Iran amemwambia ripota wa kituo cha habari cha Al-Alam kwamba nchi zote za eneo hilo zina…
Hofu ya Wazayuni juu ya uwezekano wa kurudi kwa uhusiano wa kawaida kati ya Iran na Misri
Baada ya makubaliano hayo kati ya Iran na Saudi Arabia, hivi sasa vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vinazungumzia wasiwasi na hofu ya mamlaka ya Tel Aviv kuhusu kuhalalisha uhusiano kati ya Tehran na Cairo katika siku za usoni. Kwa mujibu wa shirika la habari la Palestina “Sama”, tovuti ya habari ya “Makor Rashon”…
Mwandani Bora ni Hulka Njema – Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
Hotuba ya Ijumaa – Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi (Mkuu wa shule Jamia Urwatul Wuthqa – Lahore) Imetolewa katika msikiti wa: Masjid Baitul ul Ateeq Lahore – Pakistan Machi 10, 2023 HOTUBA YA 1: UCHA MUNGU KATIKA URITHI NI KUWATENDEA HAKI MAYATIMA. Ninawausieni nyinyi pamoja na kuiusia nafsi yangu kumcha Mwenyezi Mungu, pamoja na…
Safari ya Netanyahu nchini Ujerumani huku maandamano ya Wazayuni yakiendelea
Serikali ya Ujerumani ilitangaza kuwa kansela wa nchi hiyo atakuwa mwenyeji wa waziri mkuu wa Israel katika mkutano wa “chakula cha mchana” mjini Berlin Alhamisi hii. Afisa wa Ujerumani alitangaza mpango wa Waziri Mkuu Olaf Schultz kwa ajili ya mkutano wa pande mbili na Benjamin Netanyahu huko mjini Berlin. Vyanzo vya habari kutoka Berlin, mji…
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia: Nina hamu ya kuonana na waziri mwenzangu wa Iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Faisal bin Farhan ameelezea nia yake ya kukutana haraka na Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian, baada ya nchi hizi mbili kufikia makubaliano ya kufufua uhusiano baina yao. Akihojiwa na gazeti la Al-Sharq Al-Awsat, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia amesema:…
Idadi kubwa ya Wapalestina yatiwa nguvuni na jeshi la Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan
Vikosi vya Kizayuni vinavyoikalia kwa mabavu vilianza oparesheni ya kuvamia, kusaka na kukamata Wapalestina katika maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu kuanzia alfajiri ya leo (Jumatatu). Wanajeshi wa utawala ghasibu wa Kizayuni waliwatia mbaroni ndugu wanne waliojulikana kwa majina Muhammad, Bara, Abdul Rahman na Momin Qarawi kutoka kambi ya…
Afisa wa jeshi la Iraq: Zaidi ya wanachama 400 wa ISIS bado wako Iraq
Afisa wa jeshi la Iraq amesema kuwa kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) bado lina wapiganaji 400 hadi 500 katika nchi hiyo. Qais Al-Mohammadawi, Naibu wa Kamandi ya Operesheni ya Pamoja, ambayo inasimamia ushirikiano wa vikosi vya usalama vya Iraqi na muungano wa kimataifa, ametangaza kuwa wapiganaji wa kundi la kigaidi la ISIS nchini Iraq…