Ayatullah Sayyid Muhammad Sadiq Rouhani aaga dunia
Ayatullah Seyyed Muhammad Sadiq Rouhani, mmoja wa wanazuoni wa Chuo cha Kidini cha Qom, ameaga dunia usiku wa kuamkia leo. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, ofisi ya Ayatullah Rouhani imetoa tangazo ikieleza kwamba: Magharibi ya Ijumaa ya jana, Desemba 16, 2022, roho tukufu na iliyotukuka ya Ayatullah Seyyed Muhammad Sadiq Rouhani imeungana na…
Scotland kukabiliana na tatizo linaloongezeka la chuki dhidi Uislamu
-Katika mkutano kamili wa Baraza la Serikali za Mitaa la Eneo la Scotland, la Uingereza wiki iliyopita, diwani Ali Salamati (Kilbride Magharibi Mashariki) alileta hoja ya kuitaka mamlaka ya eneo hilo azimio la kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia. Hoja hiyo mbali na kutaka ufafanuzi kamili wa maana ya ‘Islamophobia’ ilitaka baraza hilo…
Zakzaky: Mauaji ya Zaria ni ishara ya Waislamu wa Nigeria kuwa katika njia sahihi
Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, mauaji ya umati ya Zariya yaliyofanywa na vyombo vya usalama vya nchi hhiyo ni ishara ya wazi kwamba, Waislamu wa taifa hilo wamo katika njia sahihi. Sheikh Ibrahim Zakzaky amesema hayo wakati alipokutana na familia za wahanga wa shambulio la wanajeshi wa Nigeria…
Mkutano wa kimataifa wa mazungumzo ya Uislamu na Uhindu mjini New Delhi India
Duru ya tatu ya mkutano wa kimataifa wa mazungumzo ya Uislamu na Uhindu iliyokuwa na anuani ya “Mchango wa Dini wa Kuishi Pamoja Katika Amani na Ustawi” umefanyika mjini New Delhi kwa kuhudhuriwa na makhatibu, shakhsia wenye vipawa na Maulamaa wa Iran na India. Ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulioshiriki katika mkutano huo…
Sheikh Zakzaky asimulia tukio la mauaji ya Zaria nchini katika kumbukizi ya mwaka wa saba
Katika kumbukumbu ya miaka 7 ya mauaji ya umati ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Nigeria huko Zaria, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) alisimulia matukio ya siku hizo katika mahojiano. Mwezi Disemba 2015, Jeshi la Nigeria lilivamia makazi ya Shaykh Ibrahim Zakzaky kiongozi wa Harakati ya Kiislamu katika mji wa Zaria…
Hamas: Wapalestina hawataiacha Israel itekeleze njama zake
Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema Wapalestina katu hawatouruhusu utawala haramu wa Israel utekeleza njama na mipango yake michafu dhidi ya mji mtakatifu wa Quds na Masjidul Aqsa. Ismail Haniya amesema hayo katika hotuba aliyoitoa jana Jumatatu kwa mnasaba wa kuadhimisha miaka 35 tangu ilipoasisiwa harakati…
Waandaaji wataka mawazo mapya katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran
Sekretarieti ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Tehran imesema iko tayari kupokea mawazo na mapendekezo mapya kwa ajili ya kuandaa vyema tukio la kimataifa. Sekretarieti hiyo, yenye mafungamano na Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu anayeshighulikia masuala ya Qur’ani Tukufu, imesema wale ambao wana mawazo na mapendekezo katika suala hilo wakiwemo…
Riba ni mfumo wa maisha wa kikafiri – Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi (Mkuu wa shule Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore) Imetolewa: Msikiti wa Baitul Ateeq Lahore – Pakistan Desemba 9, 2022 Hotuba ya 1: Riba ni mfumo wa maisha wa kikafiri unaowafikisha Jehanamu Ninawausieni nyinyi pamoja na kuiusia nafsi yangu kumcha Mwenyezi Mungu, na nawasisitizieni kuyasimamisha maisha yenu katika…