Ulimwengu wa Kiislamu

Indonesia yakataa kumpokea mjumbe maalumu wa kutetea ubaradhuli wa Marekani

Indonesia yakataa kumpokea mjumbe maalumu wa kutetea ubaradhuli wa Marekani

Marekani imelazimika kufuta safari ya mjumbe wake maalumu wa kutetea eti haki za mabaradhuli (LGBTQ) nchini Indonesia, baada ya nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia kusema kuwa haitampokea afisa huyo wa Washington. Baraza la Maulamaa la Indonesia jana Ijumaa lilitoa taarifa ya kupinga safari ya Jessica Stern, mjumbe maalumu wa Marekani katika masuala ya usenge, usagaji na…

Jumuiya ya Walimu wa Qur’ani yaanzishwa nchini Mauritania

Jumuiya ya Walimu wa Qur’ani yaanzishwa nchini Mauritania

Jumuiya ya walimu na wataalamu wa Qur’ani Tukufu iliyoanzishwa nchini Mauritania ilianza shughuli zake katika sherehe iliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nouakchott. Inalenga kuandaa na kuratibu shughuli za walimu na wataalamu wa Qur’ani na kuboresha hali zao ili kuwahudumia vyema wanafunzi wa Qur’ani, msemaji wa shirika hilo alisema. Akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi,…

Kongamano la Kuala Lumpur kujadili Qur’ani Tukufu inavyoweza kutatua changamoto za kisasa

Kongamano la Kuala Lumpur kujadili Qur’ani Tukufu inavyoweza kutatua changamoto za kisasa

Kongamano limepangwa kufanyika katika mji mkuu wa Malaysia Disemba 3 kujadili masuluhisho ya Qur’ani Tukufu kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za siku hizi. Taasisi ya Warisan Ummah Ikhlas Foundation (WUIF) ndiyo inayoandaa hafla hiyo kwa kushirikisha wataalamu kutoka nchi kadhaa. Wazungumzaji watatoka Malaysia, Indonesia, Bangladesh, Misri, Marekani na Palestina. Ukumbi wa Perdana MTI huko…

Wimbi jipya la mauaji ya wasomi na wanaharakati laripotiwa Saudia

Wimbi jipya la mauaji ya wasomi na wanaharakati laripotiwa Saudia

Wimbi jipya la kunyongwa na kuuliwa wasomi na wanaharakati wa masuala ya kijamii limeripotiwa nchini Saudi Arabia baada ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo kumtia nguvuni mwanazuoni wa Kiislamu katika mji mtakatifu wa Madina. Kamata kamata hiyo nchini Saudia inafanyika kwa mujibu wa sheria eti za kukabiliana na ugaidi na sheria nyingine zilizowekwa kwa…

Mmiliki wa mgahawa Ufaransa atozwa faini kwa wuwabagua Waislamu

Mmiliki wa mgahawa Ufaransa atozwa faini kwa wuwabagua Waislamu

Mahakama moja ya Ufaransa imemtoza faini mmiliki wa mgahawa kusini-magharibi mwa nchi hiyo ya Ulaya kwa kumkataza mwanamke Mwislamu kuingia akiwa amevaa mtandio wa Kiislamu, unajulikana pia kama Hijabu. Mahakama katika mji wa Bayonne katika eneo la Basque iliamua kwamba mmiliki wa mgahawa wa kike mwenye umri wa miaka 64 alikuwa na hatia ya ubaguzi…

Bin Salman anaigeuza ardhi ya maeneo matakatifu ya Makka na Madina uwanja wa ufasiki wa kimaadili

Bin Salman anaigeuza ardhi ya maeneo matakatifu ya Makka na Madina uwanja wa ufasiki wa kimaadili

Mwandishi wa habari na mpinzani wa utawala wa kifalme wa Saudi Arabia amekosoa kufanyika tamasha la muziki liitwalo MDLBEAST katika ardhi ya maeneo mawili matakatifu (Haramaini-Sharifaini) ya Makka na Madina na kueleza kwamba: Bin Salman anatoa huduma kubwa zaidi kwa maadui wa Uislamu kwa kuigeuza nchi hiyo kuwa uwanja wa kufanyia ufisadi wa kimaadili. Katika…

Hamas: Wavamizi watateketea katika moto wa hujuma dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa

Hamas: Wavamizi watateketea katika moto wa hujuma dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imewatahadharisha Wazayuni kuhusu kuendelea kuuhujumu Msikiti wa al Aqsa na kuwatolea mwito Wapalestina kuhudhuria kwa nguvu zote na kwa mshikamano katika msikiti huo. Msikiti wa al Aqsa ambao ni nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu na wa Palestina katika mji wa Baitul Muqaddas umekuwa ukilengwa na kukabiliwa…

Raisi: Iran daima inaunga mkono taifa lenye umoja na serikali yenye nguvu huko Iraq

Raisi: Iran daima inaunga mkono taifa lenye umoja na serikali yenye nguvu huko Iraq

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo kati yake na Waziri Mkuu wa Iraq hapa Tehran kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku zote inakaribisha na kuunga mkono taifa lenye mshikamano na serikali yenye nguvu huko Iraq. Mohammed Shia al Sudani Waziri Mkuu wa Iraq jana Jumanne aliwasili Tehran akiongoza ujumbe wa…