Mashabiki wa Kombe la Dunia wajifunza kuhusu Uislamu katika Msikiti wa Doha
Wahubiri wa kiume na wa kike wenye uwezo wa kuzungumza lugha kadhaa katika Msikiti wa Kijiji cha Utamaduni cha Katara katika mji mkuu wa Qatar wa Doha wanatoa maelezo kuhusu Uislamu na halikadhalika wanabainisha uvumilivu wa dini hii tukufu kwa watalii wakati wa Kombe la Dunia la 2022. Msikiti huo umekuwa kitovu cha mashabiki wa…
Noam Chomsky: Nia ya Marekani ni kuudhofisha Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Mwanafalsafa na mwanaisimu mtajika wa Marekani Noam Chomsky amethibitisha kuwa serikali ya nchi hiyo inasaidia na kuunga mkono machafuko ndani ya Iran na akabainisha kwamba Washington inaunga mkono hatua zozote za kuudhoofisha Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hivi karibuni Marekani iliiwekea vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutumia kisingizio cha kuunga mkono…
Msahafu unaonasibishwa na Imam Ali waonyeshwa mjini Lahore
Tamasha la Kimataifa la Sanaa ya Kiislamu, lililofanyika Lahore kwa kushirikisha nchi kadhaa za Kiislamu lilihitimishwa Jumapili. Iliangazia nyanja na nyanja tofauti za sanaa ya Kiislamu, pamoja na kaligrafia ya Kiislamu, Misahafu ya kale n.k. Moja ya sehemu kuu ilikuwa ni ile iliyoonyesha Misahafu adimu kurasa za maandishi ya Qur’ani yaliyoandikwa kwa mbinu ya mapambo…
Sana’a: Muungano wa Saudia ulitumia aina zote za silaha zilizopigwa marufuku nchini Yemen
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen imesema katika taarifa yake kwamba, watoto wa Yemen bado wanakabiliwa na mauaji, ulemavu na maradhi yanayosababishwa na vita na mzingiro. Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Serikali ya Kitaifa ya Wokovu ya Yemen (iliyoko Sana’a) katika taarifa yake kwa mnasaba wa Siku…
Msikiti Mkubwa Zaidi wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia Wazinduliwa nchini Oman
Waziri wa Wakfu Mohammed Said al-Ma’amari na Ayatullah Muhsin Araki, mjumbe wa Baraza Kuu la Hauza (vyuo vikuu vya Kiislamu ) Iran, walikuwa miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi. Pia kulikuwa na wanazuoni na maulamaa wa madhehebu ya Shia na Sunni kutoka Oman na nchi nyingine za Kiarabu. Msikiti wa Jami al-Salam huko Muscat…
Mashabiki wa soka waendelea kuiunga mkono Palestina katika Kombe la Dunia
Mashabiki wa soka wanaoshuhudia fainalii za mashindano ya kandanda ya Kombe la Dunia nchini Qatar wameendelea kuonyesha himaya na uungaji mkono wao kwa taifa la Palestina. Mashabiki wa soka wa mataifa mbalimbali wameonekana wakiingia viwanjani kushuhudia mechi mbalimbali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar wakiwa wamebeba bendera ya Palestina. Katika mechi iliyochezwa jana ya…
Vyombo vya habari vya Kizayuni: Waarabu wanajitenga na sisi wakati wa Kombe la Dunia na wanapinga fikra ya uhalalishaji wa mapenzi ya jinsia moja
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimesema kuwa, wakaazi wa nchi za Kiarabu duniani wanajiweka kando na sisi na wako kinyume na uhalalishaji wa mapenzi ya jinsia moja. Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni viliripoti jana (Jumanne, Novemba 22) kwamba mashabiki wanaozungumza lugha ya Kiarabu walijitenga na vyombo vya habari vya lugha ya…
Kongamano kubwa “Kwa jina la mwanamke, kwa ajili ya Irani” na ushiriki wa mabinti wa mapinduzi
Katika mkutano wa leo na waandishi wa habari wa Jumuiya ya Mabinti wa Mapinduzi, afisa wa Jumuiya hii ya alisema: “Adui na watu wanaowapigia miluzi na kuwapigia makofi ndani ya nchi wamechukizwa na harakati kubwa za kimapinduzi. Jeshi la wanawake litaonyesha uwepo wao kwa adui siku ya 10 ya Azar na sherehe kubwa ya binti…