Msemaji wa Ansarullah: Baadhi ya makundi ya Yemeni yanafaidika na kuendelea vita na umwagaji damu
Msemaji wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, baadhi ya mirengo ya ndani yenye mafungamano na Riyadh nchini Yemen yamekuwa “wafanya biashara wa vita”. “Mohammed Abdul Salam”, mpatanishi mkuu wa Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen (iliyoko Sana’a) na msemaji wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, alisema kuwa hivi sasa mpira uko katika…
Kumcha mwenyezi Mungu ipasavyo humaanisha kutumia kikamilifu uwezo na nguvu
Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi (Mkuu wa shule Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore) Imetolewa: Msikiti wa Baitul Ateeq Lahore – Pakistan 18th Nov. 2022 Hotuba ya 1: Kumcha mwenyezi Mungu ipasavyo humaanisha kutumia kikamilifu uwezo na nguvu. Ninawausieni nyinyi pamoja na kuiusia nafsi yangu kumcha Mwenyezi Mungu, na nawasisitizieni kuyasimamisha maisha yenu katika misingi…
Uingereza yasisitiza haitauhamishia ubalozi wake Quds
Kwa mara nyingine, Uingereza kutokana na mashinikizio na ukosoaji wa ndani na nje ya nchi, imesisitiza kuwa haina mpango wa kuuhamishia ubalozi wake katika mji wa Quds tukufu, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Hayo yalisemwa jana Jumatatu na Shailesh Vara, kiongozi wa ujumbe wa Bunge la Uingereza katika Jumuiya ya Kimataifa ya Mabunge (IPU) nchini Jordan,…
Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye bandari inayokaliwa kwa mabavu iliyomo mashariki mwa Yemen; Meli ya mafuta ya kigeni yatoroka
Vyanzo vya habari viliripoti mlipuko huo katika bandari ya al-Dabbah huko Hadramaut nchini Yemen, ambayo iko chini ya uvamizi wa muungano vamizi wa Saudi na Imarati. Vyanzo vya habari viliripoti mlipuko huo katika bandari ya Al-Dabbah, iliyoko mashariki mwa mji wa Makla, mji mkuu wa mkoa wa Hadhramout (Yemen Mashariki); Bandari ambayo inakaliwa na muungano…
Rais Raisi: Kushika nafasi ya kwanza katika kanda kwenye sekta ya afya ni kielelezo cha ustawi wa Iran
Rais Ebrahim Raisi amesema kushika nafasi ya kwanza katika eneo na ya kumi na tano duniani katika uga wa afya na tiba ni ishara na kielelezo cha maendeleo na ustawi wa nchi. Rais Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo alipotembelea Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu katika kikao cha tume…
Mashindano ya Kimataifa ya Qurani yamalizika Moscow, Russia
Duru ya 20 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qurani Tukufu iliyoanza Ijumaa iliyopita katika mji mkuu wa Russia, Moscow imemalizika huku washindi wakitangazwa na kutuzwa. Raia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Mostafa Hosseini ameibuka mshindi wa tatu kwenye mashindano hayo ya dunia yaliyofanyika katika Msitiki wa Jamia jijini Moscow. Nafasi ya kwanza imetwaliwa na…
Idadi ya watoto waliouawa vitani nchini Yemen yapindukia 8,000
Taasisi moja ya masuala ya sheria imetangaza kuwa, idadi ya watoto waliofanywa wahanga wa vita vya muungano vamizi wa kijeshi wa Saudia dhidi ya Yemen imeshapindukia elfu 8. Shirika la habari la Mehr limeinukuu televisheni ya al Mayadeen ikiripoti habari hiyo iliyotangazwa na taasisi ya kisheria ya “Intisaf” na kuongeza kuwa, kuna uwezekano mkubwa idadi…
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Shari bila shaka itasamabratishwa
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema lengo kuu la wachochezi wa machafuko ya hivi karibuni ni kuliingiza taifa la Iran katika medani na kuongeza kuwa: “Mchafuko hayo bila shaka yatakomeshwa na taifa kuendelea kusonga mbele kwa nguvu zaidi na ari mpya katika uwanja wa maendeleo ya nchi.” Kwa mujibu wa…