Ayatollah Sheikh Isa Qasim: Uchaguzi nchini Bahrain unalenga kuua demokrasia
Kiongozi wa Kishia wa Bahrain aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba kususia uchaguzi nchini humo ni kulinda demokrasia. Ayatullah Sheikh Isa Qassem, kiongozi wa Kishia wa Bahrain, kwa mara nyingine tena ametoa wito wa kususia uchaguzi wa wabunge na manispaa nchini humo. Kulingana na tovuti ya Manama Post, aliandika: “Mmoja wao amesema jambo lisilofaa…
Usiri wa London katika kutangaza idadi ya watoto wa Afghanistan waliouawa kinyama na jeshi la Uingereza
BBC imeripoti kuwa takriban watoto 64 wa Afghanistan waliuawa katika operesheni za jeshi la Uingereza wakati wa miaka ya vita nchini Afghanistan, ambapo serikali ya nchi hii hapo awali ilikuwa imekubali kesi 16 tu. Vyombo vya habari vya Uingereza vilitangaza kuwa, watoto wasiopungua 64 waliuawa katika operesheni za jeshi la nchi hiyo nchini Afghanistan kuanzia…
Shekhe Mkuu wa Al Azhar aungwa mkono kwa kuitisha mazungumzo baina ya Sunni na Shia
Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu (WFPIST) imekaribisha wito wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar wa kuanzisha mazungumzo kati ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Sunni. Katibu Mkuu wa WFPIST Hujjatul Islam Hamid Shahriari amemuandika barua Shekhe Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar mjini Cairo Sheikh Ahmed al-Tayyib, na kukaribisha wito…
Bin Salman ajibiwa: Kuvunjiwa heshima Haram Mbili Takatifu haliwi tena suala la ndani la Saudia
Wanaharakati wa mitandao ya kijamii wamemjibu Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia aliyedai kwamba hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo kwa kumueleza kuwa kutusi na kuvunjia heshima nchi ambayo ndani yake kuna Haram mbili za Makka na Madina haliwi suala la ndani la Saudia. Ukurasa wa…
Allamah Syed Jawad Naqvi: Quran ina maamuzi juu ya mafundisho na fatwa za madhehebu
Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi (Mkuu wa shule Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore) Imetolewa: Msikiti wa Baitul Ateeq Lahore – Pakistan 4th Nov. 2022 Khutba ya 1: Quran ina maamuzi juu ya mafundisho na fatwa za madhehebu Ninawausieni nyinyi pamoja na kuiusia nafsi yangu kumcha Mwenyezi Mungu, na nawasisitizieni kuyasimamisha maisha yenu katika misingi…
Bahrain: Tunataka mahusiano yetu na Israel yawe yenye kupigiwa mfano
Mshauri wa mfalme wa Bahrain amesema, nchi hiyo itaendeleza uhusiano wake na utawala wa Kizayuni katika kipindi cha aliekua waziri mkuu Bw. Netanyahu. “Khalid bin Ahmed Al Khalifa”, waziri wa zamani wa mambo ya nje na mshauri wa sasa wa Mfalme wa Bahrain katika masuala ya kidiplomasia, alisema kuwa Manama itaendeleza uhusiano wake na utawala…
Azimio la mwisho la maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana Ubeberu
Washiriki katika maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Ubeberu inayosadifiana na leo 4 Novemba, wamesisitiza udharura kuwepo mapambano endelevu dhidi ya njama za kuzusha fitna, ghasia na fujo. Washiriki katika maandamano ya leo ya kupinga ubeberu wa kimataifa ambao walikuwa wakipiga nara za “Mauti kwa Marekani” kuonyesha kuchukizwa kwao na siasa za kiuadui…
Saudi Arabia yatakiwa ikomeshe vitendo vya kuwanyonga kiholela wapinzani
Jumuiya na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yameelezea wasiwasi mkubwa yaliyonao kutokana na kuongezeka mno hatua za utawala wa Saudi Arabia za kuwanyonga kiholela wapinzani. Jumuiya hizo zimewatolea mwito viongozi wa Saudia na mamlaka husika katika nchi hiyo ya utawala wa kifalme zikomeshe mauaji na hukumu za kiholela za adhabu ya kifo. Mwito…