Ulimwengu wa Kiislamu

Hukumu ya Saudia Arabia dhidi ya daktari Mtunisia yapingwa na kulaaniwa vikali

Hukumu ya Saudia Arabia dhidi ya daktari Mtunisia yapingwa na kulaaniwa vikali

Taasisi ya Kitaifa ya Kuunga Mkono Muqawama na Kupinga Kuanzishwa Uhusiano wa Kawaida na utawala haramu wa Israel ya nchini Tunisia imelaani vikali hukumu ya Saudi Arabia ya kumfunga jela miaka 15 daktari mmoja wa kike raia wa Tunisia kwa kuweka video ya maandamano ya kuiunga mkono Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon. Taasisi…

Khatibu wa Msikiti wa al-Aqswa aonya kuhusiana na njama za Israel za kuiyahudisha Quds

Khatibu wa Msikiti wa al-Aqswa aonya kuhusiana na njama za Israel za kuiyahudisha Quds

Khatibu wa Msikiti wa al-Aqswa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu ameonya kuhusiana na njama za jeshi vamizi la Israel la kuuyahudisha mji wa Quds na kuudhibiti mji huo. Samahat Sheikh Ekrima Sabri Khatibu wa Msikiti wa al-Aqswa ametahadharisha piia kuhusiana na njama za kila leo za utawala vamizi wa Israel kuugawa msikiti wa al-Aqswa kiwakati na…

HAMAS: Utawala wa Kizayuni umeshindwa kukabiliana na muqawama Ukingo wa Magharibi

HAMAS: Utawala wa Kizayuni umeshindwa kukabiliana na muqawama Ukingo wa Magharibi

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, jinai za utawala wa Kizayuni za kuwaua kigaidi wanamapambano wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan hazitapunguza kasi ya kuimarika muqawama wa wananchi wa Palestina. Jana Jumapili, utawala wa Kizayuni ulimuua kigaidi Tamer al-Kilani, mmoja wa makamanda wa muqawama wanaojulikana kwa jina…

Murtadi Salman Rushdie apoteza jicho, apooza mkono baada ya kushambuliwa

Murtadi Salman Rushdie apoteza jicho, apooza mkono baada ya kushambuliwa

Duru moja ya kuaminika imesema kuwa, Salman Rushdie alipata majeraha makubwa katika shambulio la mwezi Agosti na amepoteza uwezo wa kuona jicho lake moja huku mkono wake mmoja nao ukiwa umepooza. Andrew Wylie ameliambia gazeti la lugha ya Kihispania la “El Pais” kwamba Rushdie, ambaye ana umri wa miaka 75, amepata madhara makubwa katika shambuliio…

Shambulizi la kemikali la Uturuki kaskazini mwa Iraq, je, ni kweli au uvumi?

Shambulizi la kemikali la Uturuki kaskazini mwa Iraq, je, ni kweli au uvumi?

Licha ya msisitizo wa vyanzo vya habari vinavyohusiana na PKK na baadhi ya taasisi kuhusiana na shambulio la kemikali la Uturuki kaskazini mwa Iraq, maafisa wa Ankara wamekanusha vikali suala hili. Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Halusi Akar, akizungumza na waandishi wa habari usiku wa jana Jumamosi, alidai kuwa jeshi la nchi hiyo halina silaha…

Hotuba ya Ijumaa – 21st October 2022, Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

Hotuba ya Ijumaa – 21st October 2022, Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

 Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi (Mkuu wa shule Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)  Imetolewa: Msikiti wa Baitul Ateeq  Lahore – Pakistan   Hotuba ya 1:  Tanguliza ucha Mungu katika miamala ya kiuchumi na Mwenyezi Mungu Atakujaalia elimu ya miamala salama Ninawausieni nyinyi pamoja na kuiusia nafsi yangu kumcha Mwenyezi Mungu, na nawasisitizieni kuyasimamisha maisha…

Benki ya Uganda yazindua akaunti ya kwanza inayofuata sheria za Kiislamu

Benki ya Uganda yazindua akaunti ya kwanza inayofuata sheria za Kiislamu

Benki ya Finance Trust ya Uganda imezindua akaunti ya kwanza kabisa inayofuata sheria za Kiislamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Viongozi na shakhsia mbalimbali wa Kiislamu walihudhuria hafla ya uzinduzi wa akaunti hiyo inayoitwa ‘Halal’ jana Alkhamisi katika mji mkuu Kampala. Julai mwaka huu, Baraza la Mawaziri la Uganda liliidhinisha benki za kibiashara za…

Uturuki yataka vikwazo dhidi ya Iran na Venezuela viondolewe ili kupunguza bei ya mafuta duniani

Uturuki yataka vikwazo dhidi ya Iran na Venezuela viondolewe ili kupunguza bei ya mafuta duniani

Uturuki imetoa wito wa kuondolewa vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Iran na Venezuela huku kukiwa na mzozo wa nishati duniani uliochochewa na oparesheni ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine. Ongezeko la bei ya nishati hasa petrol na gesi duniani ni chanzo cha kupanda gharama ya maisha kwa mamia ya mamilioni ya watu duniani…