Takwimu za hivi punde kuhusu uhalifu na jinai za muungano wa Saudia dhidi ya Yemen
Katika takwimu zake za hivi punde kuhusu jinai za muungano wa Saudia nchini Yemen, shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la Intisaf limeripoti kuwa zaidi ya wanawake na watoto 6,000 waliuawa kishahidi na zaidi ya 6,000 walijeruhiwa. Kwa mujibu wa Idhaa ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Fars, shirika la kulinda haki…
Vituo vya Kiislamu vya Russia vimelaani propaganda za chuki za nchi za Magharibi dhidi ya Moscow na ubaguzi dhidi ya raia wa Russia
Vituo vya Kiislamu vya Russia vyalaani mashambulizi ya kipropaganda ya Magharibi dhidi ya nchi hiyo. Wawakilishi wa taasisi na mashirika ya Kiislamu ya Russia wametoa taarifa ya kuunga mkono operesheni ya kijeshi ya nchi hiyo nchini Ukraine, wakilaani propaganda za uadui za nchi za Magharibi dhidi ya Moscow na ubaguzi unaofanywa dhidi ya raia wa…
Tarehe 15 Shaaban Hijiria Qamaria ni kumbukumbu ya kuzaliwa mwokozi wa ulimwengu, Imam Mahdi –Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake (ATF)
Nuru ya umaanawi ya uwepo wa Imam Mahdi ATF imeenea hata katika wakati huu wa “ghaiba” au kutokuwepo mtukufu huyo machoni mwa walimwengu. Kabla ya kumuumba mwanadamu, Mwenyezi Mungu aliwaambia Malaika wake: ‘Na pale Mola wako alipowaambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (al-Baqarah:30). Khalifa wa kwanza alikuwa Nabii Adam (as) na baada yake wakaja Manabii na…
Kutekelezwa oparesheni ya kuvunja mzingiro dhidi ya Yemen ndani ya ardhi ya Saudia
Brigedia Jenerali Yahya Saree, Msemaji wa Jeshi la Yemen mapema wiki hii alitangaza kuhusu kutekelezwa oparesheni ya kuvunja mzingiro dhidi ya Yemen iliyotekelezwa ndani ya ardhi ya Saudia. Kwa upande wa jiografia, oparesheni hiyo ya kuvunja mzingiro imetekelezwa huko Riyadh na pia katika maeneo ya kusini mwa Saudi Arabia yanayopakana na Yemen. Aidha kwa upande…
Waandamanaji wa Pakistan walaani shambulio la kigaidi katika Msikiti Mkuu wa Imamiyah huko Peshawar
Miji mbalimbali nchini Pakistani ilishuhudia maandamano ya kulaani shambulio la kigaidi dhidi ya waumini Mashia huko Peshawar. Baraza la Umoja wa Waislamu lilifanya maandamano makubwa katika maeneo tofauti ya nchi, hususan katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad, wakilalamikia mauaji yakikatili katika Msikiti Mkuu wa Imamiyah huko Peshawar. Mauaji hayo yalizua hisia na kumbukumbu za msururu…
Maandamano makubwa huko mjini Saada yakilaani vikwazo vya mafuta nchini Yemen
Wananchi wa mkoa wa Saada walioshiriki maandamano makubwa leo wametangaza kuwa kususia mafuta yanayotokana na mafuta dhidi ya Yemen ni uamuzi wa Marekani na jibu lao kwa kususia huko na kuzingirwa jihadi na operesheni ya “Asar Al-Yaman”. Kwa mujibu wa Idhaa ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Fars, mkoa wa Saada, leo (Jumatatu, Machi…
Bin Salman: Tuna matumaini ya kuendelezwa mazungumzo na Iran
Mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia ameeleza matumaini kuwa mazungumzo kati ya Iran na Saudi Arabia yatafikia hatua ambayo itakuwa nzuri kwa pande zote mbili na kutengeneza mustakabali mzuri kwa nchi zote mbili. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran, IRNA, Mwanamfalme wa Saudia, Mohammed bin Salman amesema kwamba Riyadh itaendelea na mazungumzo yake…
Mashambulizi dhidi ya Waislamu wa Yemen Yaendelea Saudia ikiwa mhusika mkuu
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa ndege za kivita za muungano vamizi wa Saudia huko Yemen jana ziliendelea kuyashambulia maeneo mbalimbali ya raia Waisalmu katika mikoa tofauti ya Yemen. Televisheni ya al Masira imeripoti kuwa, ndege za kivita za muungano vamizi huko Yemen zinazoongozwa na Saudi Arabia jana zilishambulia maeneo ya raia katika mikoa ya Saada…