
Kombe la Dunia Qatar, fursa kwa watu wa mataifa ya Kiarabu kuonyesha wanavyouchukia utawala wa Kizayuni wa Israel
Moja ya matukio ya kuvutia katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar ni kukataa wananchi wa mataifa mbalimbali ya Kiarabu kuhojiwa na vyombo vya habari vya Israel na vilevile kuiunga mkono Palestina dhidi ya utawala huo wa Kizayuni. Kimsingi, Kombe la Dunia ni uwanja wa kujionea mandhari za maamiliano baina ya watu; mandhari ambazo ni…

Bin Salman asherehekea Siku ya Wanawake kwa kutia mbaroni wanaharakati 100 wa kike
Shirika la Haki za Binadamu la Sanad limesema kuwa, viongozi wa Saudi Arabia wamewatia mbaroni makumi ya wanaharakati wa kike wanaopigania haki za wanawake nchini humo sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Ukatili dhidi ya Wanawake. Utawala wa kiimla wa Saudia unaendelea kukanyaga vibaya haki za wanawake. Kwa mujibu wa ripoti…

Mufti wa Oman awashukuru Waislamu kwa kuwasusia waandishi habari Wazayuni
Mufti mkuu wa Oman amewashukuru Waislamu na wale wote ambao wamekataa kuzungumza au kuhojiwa na na waandishi wa habari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakati wa Kombe la Dunia la 2022 linaloendelea nchini Qatar. Katika chapisho kwenye akaunti yake ya Twitter, Mufti Mkuu wa Oman Sheikh Ahmed Bin Hamad Al-Khalili ametoa shukrani kwa wale…

Saudia imeua Wayemen 18,000, kuharibu misikiti 1,679 tokea 2015
Shirika moja la kutetea haki za binadamu limesema watu zaidi ya 18,000 wa Yemen wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya muungano vamizi unaoongozwa Saudi Arabia katika nchi hiyo maskini ya Kiarabu mwaka 2015. Kituo cha Humanity Eye Centre for Rights and Development kimesema katika ripoti yake mpya kuwa, idadi jumla ya wahanga imefikia 47,673 katika siku 2,800…

Jeshi la Somalia lachukua udhibiti wa mji wa kimkakati wa El Dhere kutoka Al Shabab
Serikali ya Somalia siku ya Jumamosi ilitangaza kuwa jeshi la nchi hiyo limechukua tena udhibiti wa mji wa kimkakati wa El Dhere kutoka kwa kundi la kigaidi la al-Shabaab. Katika mkutano na waandishi wa habari, Abdirahman Yusuf al-Adala, naibu waziri wa habari, alisema kuwa zaidi ya magaidi 100 wa al-Shabaab, wakiwemo makamanda wao 12, waliuawa…

Onyo kali la Yemen kwa muungano wa Saudia kuhusu kuendelea kuporwa nishati ya nchi hiyo
Huku uporaji wa mafuta ya Yemen ukiwa unaendelea, Abdul Aziz bin Habtour, Waziri Mkuu wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen ametahadharisha kuwa, iwapo uporaji huo utaendelea, Wayemen watalazimika kuzilenga meli za mafuta za muungano wa Saudia. Vikosi vya jeshi la Yemen siku ya Jumatatu viliilazimisha meli ya mafuta iliyokuwa inapanga kukaribia bandari ya…

Yemen: Zaidi ya watoto elfu 4 wa Yemen wameuawa katika mashambulizi ya muungano wa Saudia
Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen imetangaza kuwa zaidi ya watoto elfu 4 wa Yemen wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya muungano vamizi unaoongozwa Saudi Arabia. Shirika la kisheria linalofuatilia matukio yanayohusiana na watoto wa Yemen limetangaza katika ripoti yake kuwa watoto elfu 4 na 17 wameuawa na wengine 4,588 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya…

Bin Salman na Bin Zayed hawana ubavu isipokuwa wa kuua watoto wa Kiyemen
Kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo faili la jinai za kivita la Muhammad bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia na Sheikh Muhammad bin Zayed Al-Nahyan Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) huko nchini Yemen linavyozidi kuwa kubwa. Licha ya vyombo vingi vya habari vya Magharibi kuelekeza macho na masikio yao…