
Yemen yalaani mauaji ya kijana Ali Atef huko Riyadh
Wizara ya Masuala ya Wageni ya Yemen imelaani mauaji yaliyofanywa na vyombo vya usalama vya Saudia dhidi ya raia wa nchi hiyo”Ali Atef Hazban Al-Ali” mjini Riyadh huku familia yake ikifichua maelezo ya kushtua ya tukio hilo. Mtandao wa Al-Alam umeripoti kuwa, familia ya “Ali Atef Hazban Al-Ali” imethibitisha katika mkutano na waandishi wa habari…

Kurejea Saudi Arabia katika mfumo wa ukandamizaji; sura halisi ya bin Salman
Katika miezi ya hivi karibuni Saudi Arabia imeingia katika hatua mpya ya vitendo vya ukatili na ukandamizaji dhidi ya wanaharakati wa kisiasa, kiraia na wa haki za binadamu. Viongozi wa utawala vamizi wa Saudi Arabia wameshadidisha utoaji wa hukumu nzito dhidi ya wanaharakati hao na hivyo kuifanya nchi hiyo kuingia katika mkondo mpya wa kushadidisha…

Upinzani wa wananchi wa India dhidi ya safari ya Bin Salman nchini humo
Miji ya New Delhi na Mumbai Jumapili ilishuhudia maandamano makubwa ya wananchi wanaopinga na kulalamikia safari ya Mohammed bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia huko India mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba. Waandamanaji walikuwa wamebeba vibonzo vya Bin Salman wakilaani mashambulizi ya jeshi la Saudia huko Yemen na ukandamizaji unaofanywa na utawala…

Haki za binadamu ya Yemen: Saudia imeua makumi ya wahajiri wa Kiafrika
Kaimu Waziri wa Haki za Binadamu wa Yemen amelaani mauaji ya wahajiri wa Kiafrika yaliyofanywa na walinzi wa mpaka wa Saudi Arabia. Mtandao wa Al-Masira nchini Yemen umepata picha zinazoonyesha kwamba, walinzi wa mpaka wa Saudi Arabia waliwaua makumi ya wahajiri wa Kiafrika kwenye mpaka wa nchi hiyo na Yemen. Ripoti hiyo imesema, Waafrika walionusurika katika…

Wanamfalme wa Saudia na biashara ya madawa ya kulevya Mashariki ya Kati
Duru moja nchini Saudi Arabia imeripoti kuhusu kuongezeka matumizi ya madawa ya kulevya na kuhusika wanamfalme wa nchi hiyo katika kuingiza nchini mihadarati. Takriban hakuna nchi iliyosalimika na janga la madawa ya kulevya hata hivyo kile ambacho kinaitofautisha Saudi Arabia katika eneo la Mashariki ya Kati ni kuhusika rasmi makademu, wanamfalme na maafisa wa nchi…

Kilichofanyika Bahrain ni uchaguzi au uteuzi tu wa watu?
Jana Jumamosi, ulifanyika uchaguzi nchini Bahrain wa kuchagua wabunge 40 wa Baraza la Wawakilishi na wajume 30 wa Mabaraza ya Miji. Maamuzi yanayopitishwa na bunge hilo la wawakilishi hayana ulazima wa kutekelezwa bali hupata nguvu ya utekelezaji yanapoidhinishwa na bunge la mashauriano inalojulikana kama Seneti, ambalo wajumbe wake wote 40 wanateuliwa na mfalme. Wagombea wote wa uchaguzi…

Upinzani Bahrain waafikiana kususia uchaguzi wa leo wa Bunge
Vyama na makundi ya upinzani nchini Bahrain yameafikiana kwa kauli moja juu ya kuususia uchaguzi wa Bunge unaotazamiwa kufanyika hii leo nchini humo. Naibu Katibu Mkuu wa mrengo mkubwa zaidi wa upinzani nchini humo wa al-Wefaq ametangaza kuwa, makundi yote ya upinzani katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi yameafikiana kususia uchaguzi huo wa leo….

“Shoka la Ibrahim” lafichua nyaraka za siri za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia
Kikundi cha mtandao kimechapisha maelfu ya hati na nyaraka za siri za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia. Serikali ya Saudia, hasa baada ya mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo, Mohammed bin Salman, kutwaa madaraka, imechukua hatua kali za kuwaandamana waandishi na wanaharakati wa haki za binadamu, makumi ya maulama, waandishi, washairi…