
Faili la pili la sauti ya mwandishi wa BBC: Lengo la ghasia ni kuigawa Iran
Faili la pili la sauti lililovuja la mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC limefichua wazi zaidi jinsi televisheni inayofadhiliwa na Saudia inayojiita ‘Iran International’ inavyoongoza kampeni ya kuigawa Iran vipande vipande. Ghasia zilizuka Iran wiki za hivi karibuni baada ya Bi. Mahsa Amini aliyekuwa na umri wa miaka 22 kuanguka katika kituo cha…

Inkstick: Silaha za Marekani zinatumika kuua raia wa Yemen
Vyombo vya habari vya Marekani vimefichua kwamba muungano wa vita unaoongozwa na Saudi Arabia unatumia silaha zilizotengenezwa Marekani kuua raia wa Yemen. Kituo cha habari cha “Inkstick” huko Marekani kimeripoti kuwa raia wasio na hatia wa Yemen wanauawa kwa silaha za Marekani na kuongeza kuwa: Mbali na mazoezi mengine yaliyofanywa katika ardhi ya Marekani, Kikosi cha Anga cha…

Watu wenye silaha wateka nyara makumi ya watu Nigeria, 11 wauawa
Watu wenye silaha nchini Nigeria wamewateka nyara takriban watu 80 na kuwaua wengine 11 katika mashambulizi tofauti huko kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo. Shirika la habari la Reuters limeripoti habari hiyo na kuwanukuu wakuu wa kimila na wakaazi wameneo hayo wakithibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, katika mashambulizi ya hivi karibuni zaidi ya magenge yenye silaha ambayo…

Kukaribia kumalizika muhula wa serikali ya muda ya Taliban nchini Afghanistan
Msemaji wa serikali ya muda ya Taliban nchini Afghanistan amesema kipindi cha uongozi wa serikali hiyo kitamalizika baada ya muda si mrefu ujao. Zabihullah Mujahid amevieleza vyombo vya habari katika mji mkuu wa nchi hiyo Kabul kwamba: juhudi mbalimbali zinaendelea kufanywa kwa ajili ya kupatikana mazingira mapya Afghanistan na serikali ya muda kuhitimisha shughuli zake. Mujahid…

Saudia yamhukumu kifo kijana kwa ‘kosa’ la kumuandalia futari mpinzani wa Ufalme
Shirika moja la kimataifa la kutetea haki za binadamu limesema mahakama ya Saudia imetoa hukumu ya kifo kwa kijana mmoja kwa ‘kosa’ la kumuandalia futari mpinzani wa ufalme katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Shirika la Umoja wa Ulaya la Haki za Kibinadamu la Saudia (ESOHR), katika ujumbe lililoweka kwenye ukurasa wake wa Twitter siku ya…

Bin Salman ajibiwa: Kuvunjiwa heshima Haram Mbili Takatifu haliwi tena suala la ndani la Saudia
Wanaharakati wa mitandao ya kijamii wamemjibu Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia aliyedai kwamba hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo kwa kumueleza kuwa kutusi na kuvunjia heshima nchi ambayo ndani yake kuna Haram mbili za Makka na Madina haliwi suala la ndani la Saudia. Ukurasa wa…

Msururu wa hukumu za vifo na kunyonga watu kwa halaiki; rekodi ya jinai aliyojiwekea Bin Salman
Shirika la Haki za Kibinadamu la Saudi Arabia lenye makao yake Ulaya limefichua kuwa viongozi wa utawala wa Riyadh wametoa hukumu ya kifo kwa wafungwa 15 walioshtakiwa kwa masuala ya kiitikadi, na kwamba kwa kutolewa hukumu hizo, idadi ya watu walio hatarini kunyongwa nchini humo imefika 53, wanane miongoni mwao wakiwa ni vijana chipukizi na…

HAMAS: Msikiti wa Aqsa uko chini ya dhulma kubwa ya Wazayuni
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, Msikiti wa al Aqsa (ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu) ni miongoni mwa nembo kuu ya Uislamu na kwamba mji mtakatifu wa Quds uliko Msikiti huo mtakatifu, daima umekuwa ukilengwa na maadui Wazayuni. Ayad Fannunah, mmoja wa viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu…