
Msafara wa baharini wa Lebanon waelekea mpaka wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu kulinda maliasili zake
Msafara wa majini wa Lebanon umeanza safari yake ya kuelekea mpaka wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) kwa lengo la kulinda utajiri wa nchi hiyo wa maliasili za mafuta na gesi dhidi ya uporaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, msafara wa majini wa Lebanon ambao uliandaliwa…

Watu 20 wauawa Somalia katika shambulio la kigaidi la al-Shabab
Watu wasiopungua 20 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia shambulio la kigaidi la al-Shabab katikati mwa Somalia. Duru za usalama zinasema kuwa, shambulio hilo la al-Shabab lililolenga mabasi kadhaa katika mji wa Hiran katikati mwa Somalia limetokea Jumamosi ya leo na kwamba, wanawake na watoto ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo. Taarifa zaidi…

Taliban: Hatuna mpango wa kuutambua rasmi utawala haramu wa Israel
Msemaji wa Ofisi ya Kisiasa ya Taliban nchini Qatar amesema kuwa, kundi hilo halina mpango wa kuutambua rasmi utawala haramuu wa Israel. Mulla Muhammad Naeem amekanusha taarifa za baadhi ya vyombo vya habari vinavyoeleza kwamba, kundi la Taliban halina tatizo na nchi yoyote ile ukiwemo utawala ghasibu wa Israel na kubainisha kwamba, amenukuliwa vibaya kwani huo…

Zaidi ya maafisa 8,000 wa polisi wa Somalia wapewa mafunzo na kikosi cha AU
Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia kimetoa mafunzo na ushauri wa kiusalama kwa maafisa polisi 8,167 wa Somalia kikosi hicho kilipotumwa kwa mara ya kwanza nchini humo mwaka 2009. Mkuu wa Polisi wa Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS), Rex Dundun amesema hayo na kuongeza kuwa, maafisa…

Muungano vamizi wa Saudia wazuia meli ya nne iliyobeba shehena ya mafuta ya Yemen
Shirika la mafuta la Yemen limetangaza kuwa, muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia umeizuia meli ya nne iliyobeba shehena ya mafuta ya nchi hiyo. Mbali na kuiba mamilioni ya mapipa ya mafuta kutoka Yemen, muungano wa kijeshi wa Saudia umeshadidisha hali mbaya ya uhaba wa mafuta na fueli katika nchi hiyo masikini na iliyoathiriwa…

Takwimu mpya za kutisha zatolewa kuhusu jinai za Saudia nchini Yemen
Wizara ya Afya ya Yemen imetangaza takwimu mpya za hasara roho na mali za watu zilizosababishwa na jinai za miaka minane ya vita vya kivamizi vya muungano wa nchi za Kiarabu wakiongozwa na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati). Mwaka 2015, Saudia na Imarati kwa baraka kamili za Marekani, nchi za Magharibi…

Nusu ya wananchi wa Saudia wanalalamikia ugumu wa maisha
Uchunguzi wa hivi karibuni kabisa wa maoni unaonesha kuwa, nusu ya wananchi wa Saudia Arabia wanalalamikia ugumu wa maisha na kupanda vibaya kwa bei za bidhaa. Kwa mujibu wa al Khalij al Jadid, uchunguzi huo wa maoni umefanywa na shirika moja la kibiashara la eneo hili baada ya kuombwa kufanya hivyo na taasisi ya Marekani…

Mshikamano kambi ya muqawama, ujumbe wa Hamas wakutana na Sayyid Nasrullah
Ujumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS umeonana na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon mjini Beirut, ukiwa ni ushahidi wa kuzidi kushikamana kambi ya muqawama katika eneo hili. Shirika la habari la Quds limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, ujumbe huo wa ngazi za juu wa HAMAS…