
Mwanamke Saudia afungwa jela miaka 34 kwa ujumbe wa Twitter
Saudi Arabia imemhukumu mwanamke mmoja kifungo cha miaka 34 jela, eti kwa kupatikana na hatia ya kumiliki ukurasa wa Twitter na kusambaza ujumbe unaoukosoa utawala wa Aal-Saud kupitia mtandao huo wa kijamii. Salma al-Shehab, 34, mama wa watoto wawili wadogo na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Leeds alikamatwa na vyombo vya usalama vya Saudia Januari…

DAESH (ISIS) wametumia asilimia 90 ya silaha za Marekani katika operesheni za kigaidi
Mtaalamu mmoja wa masuala ya kiusalama amesema, asilimia 90 ya wahanga na waathirika wa ugaidi nchini Iraq hasa katika maeneo yaliyokombolewa wameuliwa kwa silaha za Marekani. Japokuwa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh limeshindwa na kusambaratishwa katika nchi za Iraq na Syria, mabaki ya magaidi wa kundi hilo yangaliko katika nchi hizo na Marekani…

Wanachama 13 wa genge la kigaidi la al Shabab waangamizwa Somalia
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, wanachama 13 wa genge la kigaidi ukufurishaji la al Shabab wameangamizwa katika shambulio la anga lililofanywa katikati ya Somalia. Maafisa wa kijeshi wa Somalia wametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, shambulio la anga lililofanywa nchini humo dhidi ya maficho ya magaidi wa al Shabab katika mkoa wa Hiran limeua wanamgambo…

Nyayo za mafia Waisraeli katika madai ya Wizara ya Sheria ya Marekani dhidi ya IRGC
Wizara ya Sheria ya Marekani imechapisha taarifa inayodai kuwa mtu mmoja kwa jina Shahram Poursafi, ambaye wizara hiyo ilimtaja kuwa mwanachama wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), alipanga kumtumia Mmarekani mmoja kumuua John Bolton na afisa mwingine wa utawala wa Donald Trump. Madhumuni ya njama hiyo imetajwa kuwa ni kulipiza kisasi…

Sisitizo la Kiongozi Muadhamu kuhusu kuinuliwa hadhi ya Harakati ya Jihad Islami
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amejibu barua ya Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina na kusema, “mapambano (muqawama) ya kishujaa ya Jihad Islami yatapelekea kupanda hadhi ya harakati hiyo katika mapambano sambamba na kusambaratisha hadaa za utawala wa Kizayuni na kuufedhehesha utawala huo.” Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi…

Sayyid Nasrullah: Iran ndio moyo wa Uislamu na mrengo wa muqawama
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndio moyo wa Uislamu na mrengo wa muqawama wa Kiislamu duniani. Sayyid Hassan Nasrullah alisema hayo jana Jumanne mjini Beirut akiuhutubia umati wa waombolezaji wa Ashura ya Imam Hussein (AS) na kuongeza kuwa, Iran chini ya uongozi wa Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu…

AU yalaani ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza
Umoja wa Afrika (AU) umeungana na jamii ya kimataifa kulaani jinai za kinyama zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Ukanda wa Ghaza huko Palestina. Katika taarifa jana Jumapili, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Moussa Faki Mahamat amesema kushambuliwa raia na kuendelea kukaliwa kwa mabavu maeneo ya Palestina na…

Wazayuni: Jihad al Islami imeweka tayari zaidi ya makombora 3000 yakisubiri kufyatuliwa tu
Duru za Kizayuni zimedai kuwa, Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina imeweka tayari kwa ajili ya kufyatuliwa makombora zaidi 3000 baada ya kiongozi wake mmoja kukamatwa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Mapema Jumanne asubuhi, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni waliivamia kambi ya wakimbizi ya Jenin na kumuua shahidi Mpalestina mmoja na kumteka…