
Simu ya Amir Abdullahian na Bin Farhan na hali ya kukata tamaa ya Wazayuni
Mawasiliano ya simu ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na mwenzake wa Saudia na mapitio ya matukio ya hivi punde kuhusiana na makubaliano kati ya nchi hizo mbili na kuandaa mkutano wa pande hizo mbili katika mwezi wa Ramadhani. Ni msisitizo maradufu katika azma ya nchi hizo mbili ya kutekeleza makubaliano hayo ya…

Magaidi wa “Iran International” wajificha mjini London kwa kutumia anwani ya “kufanya kazi za mbali”
Baada ya kuchapishwa kwa ripoti kuhusu uhamishaji wa shughuli za mtandao wa kigaidi unaojulikana kwa jina la “Iran International”, unaofadhiliwa na Saudi Arabia, Msemaji wa mtandao huu wa kigaidi alitangaza kuwa wafanyikazi wa mtandao huu wa kigaidi wanajificha chini ya jina la kufanya kazi kwa mbali. Katika mahojiano na gazeti la Saudia la “Al-Sharq Al-Awsat”…

Kuendelea ukandamizaji wa Aal Khalifa dhidi ya wafungwa wa kisiasa katika kukaribia mwaka wa 12 wa mapambano ya wananchi
Katika kukaribia maadhimisho ya kutimia mwaka wa 12 wa mapambano ya wananchi wa Bahrain, utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain unawazuia wafungwa wa kisiasa nchini humo kuwasiliana na kuoana na familia zao katika fremu ya sera zake za ukandamizaji na kuwawekea mbinyo na vizingiti mbalimbali wafungwa wa kisiasa na wapinzani nchini humo. Mwaka…

Mtazamo mwingine kuhusu uwekezaji mkubwa wa Bin Salman katika michezo Saudia
Iwapo mtu yeyote atafuatilia habari za Saudi Arabia baada ya kunyakuliwa madaraka ya nchi hiyo ya kifalme na Mohammed bin Salman, atakumbana na mkanganyiko mkubwa katika mielekeo na sera za nchi hiyo. Moja ya matukio na mifano ya wazi katika uwanja huo ni kwamba, kwa upande mmoja, Bin Salman anataka kuonyesha sura inayoitwa ya kisasa…

Mashambulio ya Saudia mpakani mwa Yemen yameua watu saba na kujeruhi 91
Duru za Yemen zimeripotiwa kuwa, tangu ulipoanza mwaka mpya wa 2023 hadi sasa, watu saba wameuawa na wengine 91 wamejeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na utawala wa Saudi Arabia katika maeneo ya mpakani mwa Yemen. Kwa uungaji mkono wa Marekani, Muungano wa Falme za Kiarabu na nchi nyingine kadhaa, Saudi Arabia iliivamia kijeshi Yemen mwezi Machi 2015…

Sana’a: Uingereza sababu kuu ya uvamizi Yemen
Waziri Mkuu wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen ameeleza kuwa, Uingereza si tu haiwezi kusaidia kupunguza mateso na masaibu ya kiuchumi ya wananchi wa Yemen bali nchi hiyo ni sehemu kuu ya njama ya kuvamiwa nchi hiyo. James Kariuki mwanadiplomasia wa serikali ya Uingereza ambaye ni Naibu Balozi wa Kudumu wa nchi hiyo…

Wanajeshi saba wa Somalia wauawa katika shambulio la Shabab kwenye kambi ya kijeshi
Wanajeshi saba wa serikali ya Somalia wameuawa katika shambulio la jana Ijumaa lililofanywa na genge la ukufurishaji la al Shabab kwenye kambi ya kijeshi ya mji wa Somalia uliookombolewa na jeshi la Serikali wiki hii. Wizara ya Habari ya Somalia imetangaza habari hiyo na kusema kuwa, kamanda mkuu wa kijeshi ni miongoni mwa waliouawa baada…

Takriban wanawake 50 waliotekwa nyara nchini Burkina Faso wapatikana
Vyombo vya habari vimetangaza kuwa, takriban wanawake 50 waliotekwa nyara hivi majuzi kaskazini mwa Burkina Faso na watu wanaoshukiwa kuwa magaidi, wamepatikana. Shirika la habari la Burkina Faso limeripoti habari hiyo kwa kuandika: “Wanawake waliotekwa nyara na magaidi usiku wa tarehe 12-13 mwezi huu wa Januari 2023 huko Arbinda wamepatikana.” Shirika la Habari la Taifa…