
Shirika la kutetea haki za binadamu laonya, Saudia inawanyonga wafungwa kwa sababu za kiitikadi
Shirika la kutetea haki za binadamu la Sanad limetangaza kuwa limepokea taarifa zinazoonyesha nia ya Saudi Arabia ya kutekeleza hukumu za kifo kwa idadi ya wafungwa wa itikadi na wanajeshi. Shirika la hilo la Sanad limeeleza kwenye akaunti yake rasmi ya Twitter kwamba: Mahakama ya kijeshi, ambayo ilianzishwa ili kuwahukumu wafungwa wa kijeshi kutokana na…

Baraza la Usalama la UN litoa wito wa kushirikishwa kikamilifu wanawake nchini Afghanistan
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake juu ya uamuzi wa Taliban wa kuwazuia wanawake kuhudhuria masomo katika vyuo vikuu na kutoa wito wa ushirikishwa kamili na kwa dhati wanawake na wasichana nchini Afghanistan. Ni baada ya Serikali ya Taliban kusitisha elimu ya chuo kikuu kwa wanafunzi wote wa kike nchini Afghanistan, hatua ambayo…

Mashirika makubwa ya misaada yasitisha shughuli Afghanistan baada ya Taliban kupiga marufuku wafanyakazi wa kike
Mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali (NGOs) yamesitisha shughuli zake nchini Afghanistan baada ya serikali ya Taliban kupiga marufuku wanawake kufanya kazi katika mashirika hayo. Ripoti kutoka nchini humo zinasema kuwa, mashirika kadhaa makubwa ya kigeni yasiyo ya kiserikali nchini Afghanistan jana yalisimamisha shughuli za kibinadamu ikiwa ni, siku moja tu baada ya Taliban kuwazuia kuajiri…

Wavuvi wa Kiirani waliotekwa na al-Shabaab waachiwa huru baada ya miaka 8
Wavuvi 14 Wairani waliokuwa wanashikiliwa mateka na wanachama wa kundi la kigaidi la al-Shabaab nchini Somalia wamewasili nchini Iran baada ya kuachiwa huru. Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetangaza habari hiyo na kueleza kuwa, mabaharia hao waliokuwa wametekwa nyara na wanamgambo wa al-Shabaab miaka minane iliyopita wameachiwa huru kutokana na jitihada za kidiplomasia…

Al-Azhar: Hatua ya Taliban kuwazuia wanawake kusoma vyuo vikuu ni kinyume cha sheria za Kiislamu
Sheikhe Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri ameutaka utawala wa Taliban kuondoa marufuku ya elimu ya juu kwa wanawake nchini Afghanistan. Sheikhe Mkuu wa Al-Azhar , Sheikh Ahmed El-Tayeb Al-Azhar amesema amesikitishwa sana na uamuzi wa Taliban wa kuwapiga marufuku wanawake wa Afghanistan kutoendelea na masomo ya chuo kikuu. Katika taarifa yake…

Nchi za Kiislamu zalaani Taliban kuwazuia wanawake Afghanistan kusoma vyuo vikuu
Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu (OIC) imebainisha masikitiko yake kuhusu uamuzi wa utawala wa Taliban nchini Afghanistan kuwapiga marufuku wanawake kuendelea na elimu katika vyuo vikuu nchini humo. OIC imesema katika taarifa yake kwamba Katibu Mkuu wa jumuiya Hissein Brahim Taha analaani hatua hiyo. Katibu mkuu na mjumbe wake maalum walikuwa wameonya dhidi…

Vita vya kivamizi vya Saudia vimeisababishia Yemen hasara ya dola bilioni 64
Nchi maskini ya Kiarabu ya Yemen imesababishiwa hasara kubwa sana na madola vamizi yaliyoongozwa na Saudia katika vita vya miaka mingi nchini humo. Hayo yamesemwa na Kitengo cha Biashara za Nje cha Wizara ya Viwanda na Madini ya Serikali ya Wokovu wa Kitaifa yenye makao yake San’a, mji mkuu wa Yemen ambacho kimesema kwenye taarifa…

Lau milima pia ingempenda Ali ingelivunjika vipande vipande – Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi (Mkuu wa shule Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore) Imetolewa: Msikiti wa Baitul…