
Hamas: Maneva ya al Rakan al Shadid 3 ni dhihirisho la nguvu ya muqawama
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuwa maneva ya al Rakan al Shadid 3 yanayonesha nguvu ya muqawama. Hazim Qassim Msemaji wa Hamas ameeleza kuwa, maneva ya Al Rakan al Shadid 3 yaliyofanywa na chumba cha oparesheni za pamoja kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza yametilia mkazo umhimu wa hatua za pamoja za…

Haniya: Wapalestina watashadidisha mapambano dhidi ya ujenzi haramu wa Israel
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameionya Israel dhidi ya sera yake ya unyakuzi wa ardhi na kusisitiza kuwa, ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni utakabiliwa kwa nguvu kupitia muqawama. Ismail Haniya amesema hayo leo Alkhamisi akijibu matamshi yaliyotolewa na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu ajaye wa…

Waislamu wa madhehebu ya Kishia na nafasi yao ya kistratijiki duniani – Ali Akbar Raefipour
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu Mtazamo wa ulimwengu wa waumini. Hotuba ya Bw. Raefipour Shiraz tarehe 21 Januari 2016 Niwaambieni kitu ambacho kitawapa mtetemeko katika uti wa mgongo, kama ambavyo ni muhimu kwetu sisi kukijua; Asilimia 70 hadi 80 ya mafuta ya dunia yako mikononi mwa Mashia. Narudia tena; asilimia…

Bunge la Oman: Kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel ni uhalifu
Baraza la Ushauri la Oman limeikabidhi Kamati wa Kutunga Sheria na Kulinda Haki ya nchi hiyo; muswada wa marekebisho ya kifungu cha 10 cha sheria ya kuharamisha na kupiga marufuku kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel ili upasishwe rasmi. Yaqoob Bin Mohammed bin Khalifa al Harthi, Naibu Spika wa Baraza la Taifa la Ushauri (Bunge)…

Israel yakiri kuwa wazayuni 29 wameangamizwa katika mwaka unaomalizika wa 2022
Idara ya usalama wa ndani ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Shabak imekiri kuwa, Wazayuni 29 waliuawa katika operesheni za mashambulizi zilizofanywa na Wapalestina katika mwaka huu unaomalizika wa 2022. Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Shabak, hadi kufikia leo, Wapalestina wametekeleza operesheni 1933, ambapo Wazayuni 29 wameuliwa na wengine 128 wamejeruhiwa, likiwa ni ongezeko…

Erdogan: Ronaldo alikalishwa benchi Kombe la Dunia kutokana na uungaji mkono kwa Palestina
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amedai kuwa nyota wa soka wa Ureno Cristiano Ronaldo alipigwa marufuku ya kisiasa wakati wa michuano ya Kombe la Dunia ya FIFA ya 2022 iliyomalizika hivi karibuni nchini Qatar kwa kuunga mkono Palestina. Akizungumza katika hafla na vijana katika jimbo la Erzurum mashariki mwa nchi hiyo siku ya Jumapili,…

Wabahrain waandamana kulalamikia kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel
Wananchi wa Bahrain wameandamana kulalalamikia na kulaani hatua ya nchi yao ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel. Maandamano hayo makubwa yaliyofanyika katika mji mkuu Manama yalishuhudia waandamanaji wakiwa wamebeba mabango na maberamu huku wakipiga nara za kuulaani utawala ghasibu wa Israel unaofanywa mauaji kila leo huko Palestina inayokaliwa kkwa mabavu. Waandamanaji…

Utawala wa Kizayuni wazamisha Ukanda wa Gaza Kwa kufungua njia za maji
Usiku wa kuamkia Jumamosi, utawala wa Kizayuni ulilowesha makumi ya nyumba na mamia ya hekta za ardhi ya kilimo katika eneo hilo kwa kufungua mifereji ya maji ya mvua nyuma ya ukanda wa mpaka ulioko mashariki mwa Ukanda wa Gaza. Shirika la habari la Palestina la “Ma’an” liliripoti, likinukuu chanzo cha ndani: “Mafuriko yaliyosababishwa na…