Onyo la Tel Aviv kwa Wazayuni kuhusu safari ya kwenda nchini Qatar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia
Makao makuu ya utawala wa Kizayuni yamewashauri wakazi wa maeneo hayo yanayokaliwa kwa mabavu kutosafiri hadi Qatar kutazama michezo ya Kombe la Dunia kutokana na vitisho vya usalama. Wakati wa michezo ya Kombe la Dunia inayofanyika nchini Qatar, Makao Makuu ya Kupambana na Ugaidi ya Kizayuni jana (Jumapili) yalitoa taarifa na kuwashauri Wazayuni wasisafiri kwenda…
Pigo jingine kwa Wazayuni, Morocco yasherehekea kwa bendera ya Palestina, kupanda Kombe la Dunia
Katika hali ambayo serikali ya Morocco imetangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu na ya Waislamu, wamezidi kuonesha kutokubaliana na uamuzii huo wa utawala wa kifalme wa Morocco. Baada ya kufanikiiwa kupanda kwenye awamu ya mtoano ya mashindano ya Kombe la Dunia la Kandanda 2022 yanayoendelea…
Ripoti kuhusu jinai za kivita za muungano wa Saudia na Imarati nchini Yemen
Kituo cha sheria cha Ain al-Insaniyah (Jicho la Ubinadamu) cha Yemen kimetoa takwimu za kushtua kuhusu maafa ya kibinadamu na kiwango cha uharibifu uliosababishwa na mashambulio ya muungano vamizi wa Saudia na Imarati katika nchi hiyo, takwimu ambazo zinaanika wazi wigo wa jinai za kivita zilizofanywa na muungano huo na waungaji mkono wake wa Magharibi…
Wazayuni wameshaua shahidi Wapalestina 205 tangu mwanzoni mwa 2022
Wizara ya Afya ya Palestina imetoa ripoti yake na kusema kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022 hadi hivi sasa, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshaua shahidi Wapalestina 205 katika sehemu mbalimbali za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Wizara ya Afya ya Palestina aidha imesema kwenye ripoti yake hiyo ya jana Jumanne kwamba,…
Kanali ya Kizayuni: Israel inakabiliwa na Intifadha mpya ya Wapalestina
Chombo kimoja cha habari cha Kizayuni kimesema hali ya usalama katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu ni ya ‘hatari’ na kwamba Tel Aviv inakabiliwa na Intifadha mpya ya Wapalestina. Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Kanali ya 12 ya Kizayuni, tangu kuanza kwa operesheni za hivi karibuni katika…
Russia, Uchina zalaani ‘matumizi ya nguvu kupita kiasi’ ya Israel dhidi ya Wapalestina
Russia na China zimeulaani vikali utawala wa Israel kutokana na utumiaji wake mabavu kupita kiasi dhidi ya Wapalestina huku hali ya wasiwasi ikiongezeka katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Akizungumza katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, likiwemo suala la Palestina, siku ya Jumatatu, naibu balozi wa…
Mzayuni Ben-Gvir asema ataushambulia msikiti wa al Aqsa, HAMAS yamjibu kuwa atashindwa!
Itamar Ben-Gvir, mzayuni mwenye misimamo ya kufurutu mpaka na kiongozi wa chama cha Nguvu ya Kiyahudi ambaye amependekezwa kuwa waziri wa usalama wa ndani katika baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu, ametangaza kuwa, mnamo siku chache zijazo ataushambulia Msikiti wa Al-Aqsa. Kwa mujibu wa tovuti ya Falastin Al-Yum, Ben-Gvir, amesisitiza katika mahojiano ya televisheni akisema:…
Wapalestina waunga mkono Timu ya Soka ya Iran kabla ya mchuano wa Kombe la Dunia na Marekani
Mashabiki wa soka wa Palestina wameonyesha uungaji mkono mkubwa kwa timu ya taifa ya kandanda ya Iran, iliyopewa jina la utani la Team Melli, kabla ya mechi muhimu ya Kombe la Dunia dhidi ya Marekani leo usiku. Mashabiki wa soka wa Palestina na Iran walikusanyika katika hafla moja katika mji mkuu wa Qatar wa Doha,…