Wapalestina pawatatu wakiwemo ndugu wawili wa kiume wauliwa shahidi Ukingo wa Magharibi
Wapalestina watatu wakiwemo ndugu wawili wa kiume Jawaad na Dhaafar Abdurrahman wameuawa shahidi asubuhi ya leo baada ya kupigwa risasi na askari katili wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika kijiji cha Kafr Ain kaskazini mwa Ramallah, Ukingo wa Magharibi Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Duru za Palestina zimeripoti kuwa Dhaafar Abdurrahman Rimawi mwenye umri…
Kombe la Dunia Qatar, fursa kwa watu wa mataifa ya Kiarabu kuonyesha wanavyouchukia utawala wa Kizayuni wa Israel
Moja ya matukio ya kuvutia katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar ni kukataa wananchi wa mataifa mbalimbali ya Kiarabu kuhojiwa na vyombo vya habari vya Israel na vilevile kuiunga mkono Palestina dhidi ya utawala huo wa Kizayuni. Kimsingi, Kombe la Dunia ni uwanja wa kujionea mandhari za maamiliano baina ya watu; mandhari ambazo ni…
Wazayuni: Katika Kombe la Dunia la Qatar, tumejua ni kiasi gani tunachukiza
Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limeashiria matatizo makubwa yanayowakumba waandishi wa habari wa utawala wa Kizayuni katika mashindano ya Kombe la Dunia 2022 yanayoendelea hivi sasa nchini Qatar na kuandika, katika mashindano haya tumeelewa ni kiasi gani hatupendwi na tunachukiza vibaya katika ulimwengu wa Kiarabu. Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, gazeti…
Bin Salman asherehekea Siku ya Wanawake kwa kutia mbaroni wanaharakati 100 wa kike
Shirika la Haki za Binadamu la Sanad limesema kuwa, viongozi wa Saudi Arabia wamewatia mbaroni makumi ya wanaharakati wa kike wanaopigania haki za wanawake nchini humo sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Ukatili dhidi ya Wanawake. Utawala wa kiimla wa Saudia unaendelea kukanyaga vibaya haki za wanawake. Kwa mujibu wa ripoti…
Mufti wa Oman awashukuru Waislamu kwa kuwasusia waandishi habari Wazayuni
Mufti mkuu wa Oman amewashukuru Waislamu na wale wote ambao wamekataa kuzungumza au kuhojiwa na na waandishi wa habari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakati wa Kombe la Dunia la 2022 linaloendelea nchini Qatar. Katika chapisho kwenye akaunti yake ya Twitter, Mufti Mkuu wa Oman Sheikh Ahmed Bin Hamad Al-Khalili ametoa shukrani kwa wale…
Jumuiya 198 za Palestina na za kimataifa zatoa mwito kwa ICC kuchunguza jinai za Israel
Makumi ya asasi za Palestina na za kimataifa zimeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ifanye uchunguzi kuhusu jinai zinazofanywa na Wazayuni dhidi ya wananchi wa Palestina. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Falastin al-Yaum, jumuiya 198 za Palestina na za kimataifa zimemtaka Karim Khan, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai na…
Mashabiki wa Tunisia wanaunga mkono Palestina wakati wa Mechi ya Kombe la Dunia la 2022
Mashabiki wa Tunisia walipeperusha bendera ya “Palestine Huru” katika dakika ya 48 ya mechi yao ya Kombe la Dunia la Qatar dhidi ya Australia siku ya Jumamosi, wakimaanisha kile kinachojulikana na Waarabu kama Nakba ya 1948 wakati mamia ya maelfu ya Wapalestina walipotimuliwa kutoka nchi yao na wanamgambo wa Kizayuni na baada ya hapo ukanduwa…
Walowezi wa Kizayuni wachoma moto magari ya Wapalestina katika mji wa Quds
Walowezi wa Kizayuni wameendelea kufanya vitendo vyao vya kinyama dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina ambapo wamechoma moto magari kadhaa ya Wapalestina katika mji wa Quds. Vitendo hivyo vya kinyama ambavyo vimeongezeka mno katika miezi na majuma ya hivi karibuni jana vilishuhudiwa tena baada ya vitongoji kadhaa vya mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu kushuhudia…