Kuongezeka watoto wa Kipalestina katika magereza ya Israel
Wizara ya Mateka na Wafungwa wa Kipalestina Walioachiliwa Huru kutoka gerezani imetangaza kuwa, hivi sasa kuna watoto 170 wa Kipalestina katika magereza ya Israel huku watano kati yao wakishikiliwa pasi na kuelezwa tuhuma na makosa yao. Takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa, katika hali ya wastani watoto na mabarobaro zaidi ya 1000 wa Kipalestina hutiwa mbaroni kila…
Shtayyeh: Serikali mpya ya Israel inajiandaa kutangaza vita dhidi ya Wapalestina
Waziri Mkuu wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema, serikali mpya ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel chini ya uongozi wa wanasiasa wa mrengo wa kulia wenye misimamo ya kufurutu ada inajiandaa kutangaza vita dhidi ya Wapalestina. Kwa mujibu wa shirika la habari la Palestina SAMA, Muhammad Ashtiyeh, amebainisha kuwa mazungumzo ya uundaji baraza la…
UN yaalani mashambulizi ya kinyama ya walowezi na wanajeshi wa Kizayuni huko al Khalil
Umoja wa Mataifa umelaani mashambulizi ya kinyama ya walowezi wa Kizayuni wakishirikiana na wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel huko katika mji wa al Khalil. Wanajeshi na walowezi wa Kizayuni kila siku hushambulia maeneo mbalimbali ya Palestina kwa lengo la kufanikisha malengo yao ya kujitanua na hivyo kuwauwa shahidi, kuwajeruhi na kuwatia mbaroni raia wa…
Hamas yalaani hujuma ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Syria
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ametoa taarifa akilaani mashambulio ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Syria. Shirika rasmi la habari la Syria (SANA) limeripoti kujiri mashambulizi mapya ya anga ya utawala wa Kizayuni dhidi ya ardhi ya nchi iyo yaliyouwa wanajeshi wanne na kumjeruhi mwingine mmoja….
Hamas: Mpango wa wavamizi wa Kizayuni huko al Khalil utashindwa
Sambamba na kupongeza muqawama na mapambano ya wananchi dhidi ya utawala ghasibu wa Israel, msemaji wa harakati ya Hamas amesisitiza kuwa, juhudi za utawala wa Kizayuni za kuimarisha ujenzi wa vitongoji vya walowezi huko al Khalil hazitafanikiwa. Hali ya sasa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu hususan katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni tata mno, ambapo…
Kivuli cha ufashisti kwenye bunge na baraza jipya la mawaziri la utawala wa Israel
Siku ya Jumanne Novemba 15, kilifanyika kikao cha kwanza cha Bunge la Kizayuni (Knesset) ambapo wawakilishi 120 wa bunge hilo walikula kiapo mbele ya Isaac Herzog, rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Kati ya wabunge 120 wa Knesset, wanachama 23 pekee ndio wapya na waliosalia ni wabunge wa zamani ambao walibaki kwenye nafasi zao katika…
Wapalestina wapata ushindi mwingine Umoja wa Mataifa
Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa imepasisha azimio ikitambua haki ya watu wa Palestina ya kuamua hatima yao wenyewe. Rasimu ya azimio hilo iliwasilishwa na Misri ikishirikiana na serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika Umoja wa Mataifa, kwa niaba ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC)….
Indhari ya UNRWA kuhusu kuongezeka umaskini miongoni mwa wakimbizi wa Kipalestina
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) limetahadharisha kuhusu kuongezeka kwa kiasi kikubwa umaskini miongoni mwa wakimbizi wa Kipalestina huko Syria, Lebanon na Ukanda wa Ghaza. Wapalestina zaidi ya milioni 6 wanaishi kama wakimbizi katika nchi mbalimbali na hasa katika nchi zinazopakana na Palestina. Wakimbizi hao wa Kipalestina ambao kabla ya…