Wanamuqawama watekeleza oparesheni huko Ukingo wa Magharibi; Wazayuni 2 waangamizwa
Duru za habari zimeripoti kuwa, wanamuqawama wa Palestina wametekeleza oparesheni dhidi ya Uzayuni karibu na kitongoji kimoja cha walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Gazeti la Kizayuni la Yediot Aharonot limetangaza leo Jumanne kwamba, walowezi wawili wa Kizayuni wameangamizwa na wengine watatu wamejeruhiwa katika oparesheni ya kimuqawama iliyofanywa na kijana Mpalestina…
Utawala wa Kizayuni; kizuizi kikuu cha uwepo wa Asia Magharibi pasina silaha za maangamizi ya umati
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameutaja utawala wa Kizayuni kuwa kizuizi kikuu cha uwepo wa Asia Magharibi isiyokuwa na silaha za maangamizi ya umati. Utawala wa Kizayuni ambao unamiliki silaha za nyuklia ambapo kwa mujibu wa ripoti nyingi za kuaminika hivi sasa unamiliki vichwa vya nyuklia kati ya 200 hadi…
Wazayuni waingiwa na hofu baada ya Netanyahu kupewa jukumu la kuunda serikali mpya Israel
Sambamba na Benjamin Netanyahu kupewa jukumu la kuunda baraza la mawaziri la serikali mpya ya Israel, mmoja wa majenerali wa Israel ameutaja uteuzi wake kuwa ni maafa makubwa. Jenerali Amos Gilad wa Israel na mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama na Siasa ya Wizara ya Vita ya utawala huo ameutaja uteuzi wa mawaziri wa serikali ijayo…
Hizbullah: Marekani imekusudia kuingamiza kabisa Lebanon
Naibu wa Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani inapanga njama za kuiangamiza kabisa kabisa Lebanon. Tovuti ya al Nashra imeripoti habari hiyo na kumnukuu Sheikh Ali Da’mush akisema hayo jana Jumapili na kusisitiza kuwa, muqawama hivi sasa ni imara na una nguvu zaidi kuliko wakati mwingine wowote na kwa…
Jeshi la Israel lampiga risasi na kumuua shahidi binti wa Kipalestina
Wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamemuua shahidi msichana wa Kipalestina aliyekuwa na umri wa miaka 19 katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti habari hiyo na kueleza kuwa, binti huyo aliyetambuliwa kwa jina la Sana Al-Tal, ameuawa shahidi kwa kumiminiwa risasi na askari wa utawala…
Mrithi wa Ufalme Bahrain apewa mwaliko na Netanyahu
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa zamani wa Israel anayetazamiwa kuunda serikali mpya ya utawala wa Kizayuni amemualika Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Bahrain, Salman bin Hamad Aal Khalifah kuitembelea ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kupachikwa jina la Israel. Gazeti la The Times of Israel limeripoti kuwa, Netanyahu jana Jumapili alizungumza kwa njia…
Hamas yasisitiza kutekeleza Tangazo la Algeria na kuhitimisha hitilafu za ndani
Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza kuwa harakati hiyo ipo tayari kutekeleza Tangazo la Algeria kuhusu mapatano ya kitaifa na kuhitimisha hitilafu za ndani. Abu Marzouq amesisitiza kuwa, Hamas ina hamu na iko tayari ili kuhakikisha kuwa umoja wa kitaifa unapatikana na Tangazo la Algeria linatekelezwa. Amesema, marhala ya sasa…
“Shoka la Ibrahim” lafichua nyaraka za siri za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia
Kikundi cha mtandao kimechapisha maelfu ya hati na nyaraka za siri za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia. Serikali ya Saudia, hasa baada ya mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo, Mohammed bin Salman, kutwaa madaraka, imechukua hatua kali za kuwaandamana waandishi na wanaharakati wa haki za binadamu, makumi ya maulama, waandishi, washairi…