Wazayuni wakasirishwa na uamuzi wa Umoja wa Mataifa wenye maslahi na Wapalestina
Kamati ya Kupambana na Ukoloni ya Umoja wa Mataifa imepasisha muswada wa Kipalestina ambao ndani yake unataka rai na maoni ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuhusiana na hatua ya utawala wa Kizayuni wa israel ya kuendelea kuikalia kwa mabavu Palestina. Azimio hilo ambalo limepasishwa katika makao makuuu ya Umoja wa Mataifa mjini New…
Qatar yasisitiza tena kupinga kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel
Serikali ya Qatar kwa mara nyingine tena imesisitiza msimamo wake wa kupinga kuanzisha uhusiano wa kawaida wa aina yoyote ile na utawala wa Kizayuni wa Israel unaofanya mauaji kila leo huko Palestina. Duru za habari za Kizayuni zimetangaza kuwa, serikali ya Qatar haitaki kabisa kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israela na kwamba, Dohha inaendelea kusisitiza…
Magadi 97 wa Al-Shabaab waangamizwa nchini Somalia
Wizara ya Habari ya Somalia imetangaza mapema leo kuwa kuwa magaidi 97 wa al-Shabaab wameuawa wakati wa operesheni mbili ziilizotekelezwa na jeshi la nchi hiyo na vikosi vya usalama katika mikoa ya Galguduud na Shabelle ya Chini. Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Somalia (SUNA), Wizara ya Habari imeelzea katika taarifa kwamba magaidi…
Faili la pili la sauti ya mwandishi wa BBC: Lengo la ghasia ni kuigawa Iran
Faili la pili la sauti lililovuja la mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC limefichua wazi zaidi jinsi televisheni inayofadhiliwa na Saudia inayojiita ‘Iran International’ inavyoongoza kampeni ya kuigawa Iran vipande vipande. Ghasia zilizuka Iran wiki za hivi karibuni baada ya Bi. Mahsa Amini aliyekuwa na umri wa miaka 22 kuanguka katika kituo cha…
Utawala wa Kizayuni wakataa kukabidhi maiti za Wapalestina 10 waliouawa shahidi
Kamati inayoshughulikia masuala ya Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye magereza ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel imetangaza kuwa utawala huo ghasibu unaendelea kuzuia viwiliwili vya Wapalestina kumi waliouawa shahidi. Kwa mujibu wa chaneli ya habari ya Quds Al-Akhbariya, Kamati ya Wafungwa wa Palestina imetangaza katika taarifa yake siku ya Alkhamisi kwamba Wapalestina hao waliuawa shahidi wakati…
Qatar imewanasa majasusi kadhaa wa Israel raia wa India
Shirika la Intelijensia la Qatar limewakamata maafisa wanane wa zamani wa Jeshi la Wanamaji wa India nchini Qatar wanaoshukiwa kufanya ujasusi kwa manufaa ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel. Kwa mujibu wa tovuti huru ya habari Al-Watan, maafisa hao wanane wa zamani wa Jeshi la Wanamaji la India waliajiriwa na kampuni binafsi nchini Qatar iitwayo…
Wapalestina wakosoa njama za Kuyahudisha mtaala wa shule katika jiji la Quds
Wapalestina wanaendelea kulaani vikali njama za utawala haramu wa Israel za Kuyahudisha na kupotosha ukweli katika vitabu vya shule katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo. Kamati ya Quds ya Baraza la Wananchi la Wapalestina Nje ya Nchi imelaani mitaala potofu ya Israel iliyowekwa kwa ajili ya wanafunzi wa Kipalestina katika…
Abbas: Haina maana kuwa na nchi ya Palestina bila ya Quds, Gaza na Ukingo wa Magharibi
Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesisitiza kuwa, haitakuwa na maana yoyote kuwa na nchi ya Palestina bila ya Baitul Muqaddas (Jerusalem), Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Abbas, ameyasema hayo katika hotuba aliyotoa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 18 wa kifo cha Yasser Arafat, Rais wa zamani…