Kundi la ‘Arin al Usud laapa kuendelea na muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel
Kundi la mapambano ya Kiislamu la ‘Arin al Usud (Pango la Simba) linaloendesha mapambano yake katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina limesisitiza kuwa, watu wanaodhani kuwa muqawama umeshindwa, wanajidanganya. Kundi la muqawama wa Kiislamu la ‘Arin al Usud lilitangaza uwepo wake mwezi Aprili mwaka huu na kuyataka makundi mengine ya Palestina yaliunge…
Kushamiri kuwepo kijeshi Wazayuni kusini mwa Yemen; njama iliyoandaliwa na Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE)
Wakati hali ya mchafukoge wa kisiasa kusini mwa Yemen ikiwa imefikia kiwango cha juu huku serikali tegemezi na kibaraka iliyoko huko ikiwa haina mamlaka yoyote ya uendeshaji wa mambo yake, katika njama iliyoratibiwa na Muungano wa Falme za Kiarabu Imarati, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umeshamirisha kuwepo kwake kijeshi katika eneo hilo la kusini…
Hamas: Risasi za wanamapambano wa Palestina ni jibu kwa vitendo kwa jinai za Israel
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imesema kuwa, risasi zilizopigwa na wapiganaji ukombozi wa Palestina katika operesheni ya kulipiza kisasi karibu na makazi haramu ya walowezi katika eneo la kusini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni jibu la kivitendo kwa jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina. Msemaji…
Ukosoaji mkali wa Putin kwa mauaji ya kigaidi ya shahidi Luteni Jenerali Soleimani
Akizungumza juzi Alhamisi katika Kongamano la Valdai, Rais Vladmir Putin wa Russia amekosoa mfumo na siasa za Magharibi na kueleza kuwa nchi za Magharibi zilimuua Luteni Jenerali Soleimani; katika hali ambayo shakhsia huyo alikuwa kiongozi rasmi nchini mwake na kuongeza kwamba Wamagharibi si tu hawajakana jambo hilo bali wanajifakharisha nalo. Putin amesema: “Wao ndio walimuua…
Russia: Marekani na Ulaya zinataka kuwafanya walimwengu waghafilike na kadhia ya Palestina
Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Marekani na Ulaya ndio wahusika wakuu wa kushadidi mgogoro wa Palestina. Vasily Nebenzya, Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, umewadia wakati sasa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchuukua hatua za kurekebisha hali…
Mashabiki wa Celtic waunga mkono mapambano ya ukombozi ya watu wa Palestina
Mashabiki wa timu ya kandanda ya Celtic huko Scotland wamebeba na kupeperusha bendera za Palestina katika mechi iliyochezwa jana dhidi ya timu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine, wakitangaza uungaji mkono wao kwa Wapalestina wa eneo la Nablus wanaoendelea kukandamizwa na utawala haramu wa Israel. Kwa siku ya 16 mfululizo, wanajeshi wa Israel wanauzingira mji wa…
Kuzingirwa Nablus, ishara ya utawala wa Kizayuni kushindwa kuzima mapambano ya Palestina
Katika kuendeleza harakati zao za chuki dhidi ya Wapalestina, askari wa utawala haramu wa Israel wamekuwa wakiuzingira kwa muda sasa mji wa Nablus, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa mji huo. Siku 17 zimepita tangu kuzingirwa mji huo na askari wa utawala unaokaliwa kwa mabavu mji…
Askari wa Israel awasihi vijana Wapalestina Al-Khalil: ‘Basi tena, tutaabani’
Mitandao ya kijamii imesambaza video inayomuonyesha askari mmoja wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel akiwasihi vijana Wapalestina katika eneo la Al-Khalil, Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan wahitimishe muqawama na mapambano dhidi yake yeye na wanajeshi wenzake. Katika video hiyo ambayo imeangaliwa na watu wengi sana, anaonekana askari wa utawala wa Kizayuni akiwataka vijana…