Uyahudi

Nasrullah: Macho na makombora yetu yameelekezwa kwenye medani ya gesi ya Karish

Nasrullah: Macho na makombora yetu yameelekezwa kwenye medani ya gesi ya Karish

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah, amesema leo Jumamosi kwamba macho na makombora ya harakati hiyo yameelekezwa kwenye medani ya gesi ya Karish, ambao inazozaniwa baina ya Lebanon na utawala haramu wa Israel. Sayyid Nasrullah amesema katika hotuba yake kwa njia ya televisheni kuwa “haiwezekani kuruhusu uchimbaji wa mafuta na gesi…

Iran: Utawala haramu wa Israel siku zote umekuwa tishio dhidi ya amani na usalama wa kimataifa

Iran: Utawala haramu wa Israel siku zote umekuwa tishio dhidi ya amani na usalama wa kimataifa

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, misingi ya utawala wa kibaguzi wa Israel imejengeka juu ya uvamizi na tishio kwa amani na usalama wa dunia. Akiashiria mauaji ya Sabra na Shatila yaliyofanywa na utawala dhalimu wa Israel huko Lebanon katika kambi za wakimbizi wa Kipalestina mwaka…

Israel yamfuta kazi balozi wake anayetuhumiwa kuwabaka wanawake nchini Morocco

Israel yamfuta kazi balozi wake anayetuhumiwa kuwabaka wanawake nchini Morocco

Utawala haramu wa Israel umelazimika kumfuta kazi balozi wake wa nchini Morocco anayekabiliwa na kashfa za ngono na kuwanyanyasa kijinsia wanawake wa nchi hiyo ya Kiarabu. Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya utawala ghasibu wa Israel imetangaza kuwa, imemsimamisha kazi David Govrin balozi wake mjini Rabat na nafasi yake imechukuliwa na mwanamama Alona Fischer. David…

Hamas: Tunatazamia kuwa na uhusiano imara na Syria

Hamas: Tunatazamia kuwa na uhusiano imara na Syria

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kuwa inataka kuwa na uhusiano imara na Syria ikiwa ni katika fremu ya uamuzi wa harakati hiyo wa kuanzisha tena uhusiano na Damascus. Katika taarifa iliyoitoa leo Alhamisi, Hamas imelaani mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni huko Syria na kusisitiza kuwa harakati hiyo iko imara…

HAMAS yataka makubaliano ya Oslo baina ya PLO na Israel yafutwe

HAMAS yataka makubaliano ya Oslo baina ya PLO na Israel yafutwe

Sambamba na kutimia mwaka wa 29 tangu yaliposainiwa Makubaliano ya Oslo, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeitaka Mamlaka ya Ndani ya Palestina itangaze kufutwa makubaliano hayo ya nakama. Makubaliano ya Oslo yalitiwa saini tarehe 13 Septemba 1993 kati ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO);…

Wapalestina 2 wauawa shahidi, Mzayuni aangamizwa Ukingo wa Magharibi

Wapalestina 2 wauawa shahidi, Mzayuni aangamizwa Ukingo wa Magharibi

Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limewaua shahidi vijana wawili wa Kipalestina kwa kuwapiga risasi kaskazini mwa eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu. Jeshi la Israel limesema katika taarifa kuwa, Wapalestina hao wawili wameuawa mapema leo katika kituo cha upekuzi wa usalama karibu na kijiji cha Jalamah, kaskazini mwa…

Qatar yakataa ombi la kuanzishwa ubalozi wa Israel mjini Doha kwa ajili ya Kombe la Dunia

Qatar yakataa ombi la kuanzishwa ubalozi wa Israel mjini Doha kwa ajili ya Kombe la Dunia

Serikali ya Qatar imetangaza kukataa ombi la utawala haramu wa Israel la kuanzishwa ubalozi mdogo wa muda wa Israel mjini Doha katika kipindi cha kufanyika fainali za soka za Kombe la Dunia. Vyombo vya habari vya utawala ghasibu wa Israel hivi karibuni viliripoti kuwa, kumekuweko mazungumzo baina ya viongozi wa utawala huo na wenzao wa…

Mateka 73 wa Kipalestina wafa shahidi katika jela za utawala wa Kizayuni kwa kukosa matibabu

Mateka 73 wa Kipalestina wafa shahidi katika jela za utawala wa Kizayuni kwa kukosa matibabu

Taasisi ya kutetea haki za binadamu ya Palestina imetangaza kuwa, tangu mwaka 1967 hadi sasa Wapalestina 73 wameaga dunia kutokana na upuuzaji unaofanywa na Israel wa kutowapatia matibabu stahiki mateka wa Kipalestina katika jela za utawala huopandikizi unaozikalia kwa mabavu ardhi za Palestina. Klabu ya wafungwa ya Palestina jana Jumapili imeripoti kuwa, raia hao 73…