Taliban: Hatuna mpango wa kuutambua rasmi utawala haramu wa Israel
Msemaji wa Ofisi ya Kisiasa ya Taliban nchini Qatar amesema kuwa, kundi hilo halina mpango wa kuutambua rasmi utawala haramuu wa Israel. Mulla Muhammad Naeem amekanusha taarifa za baadhi ya vyombo vya habari vinavyoeleza kwamba, kundi la Taliban halina tatizo na nchi yoyote ile ukiwemo utawala ghasibu wa Israel na kubainisha kwamba, amenukuliwa vibaya kwani huo…
Israel imewaua Wapalestina zaidi ya 110 Mwaka huu
Jeshi katili la utawala haramu wa Israel limeua Wapalestina zaidi ya 110 na kuwajeruhi wengine wengi hadi sasa mwaka huu. Katika taarifa, Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Palestina, limesema “Hadi sasa mwaka huu, mashambulizi ya Jeshi la Utawala wa Israel yamewaua Wapalestina 111, watoto 24 na wanawake 8.” Aidha taarifa hiyo imebaini kuwa,…
HAMAS: Vita dhidi ya Israel vitaendelea mpaka mateka wote wa Kipalestina watakapoachiliwa huru
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesisitiza kuwa, vita dhidi ya utawala haramu wa Israel vitaendelea mpaka pale mateka wote wa Kipalestina wanaoshikiliwa na utawala huo ghasibu watakapoachiliwa huru. Hayo yameelezwa na Zaher Jabarin, afisa wa Hamas anayeshughulikia faili la mashahidi na mateka wa Palestina na kueleza kwamba, harakati hiyo haitapata utulivu na…
Israel yaua shahidi Wapalestina 2; yashambulia Syria kwa makombora
Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendeleza jinai na chokochoko zake dhidi ya mataifa mawili ya Waislamu katika eneo hili la Asia Magharibi. Wanajeshi makatili wa utawala huo pandikizi wamewaua shahidi mabarobaro wawili wa kiume wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Kituo cha Habari cha Palestina kimeripoti kuwa, vijana hao wa Kipalestina Yazan Afana…
Sheikh Issa Qassim: Kujengwa kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi Manama ni jinai
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain amekosoa viikali uamuzi wa utawala wa Aal Khalifa wa kuanzisha kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi katika mji mkuu Manama na kueleza kwamba, hatua hiyo ni jinai na dhulma ya wazi dhidi ya wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu. Sheikh Issa Qassim, kiongozi wa kimaanawi wa Mapinduzi ya Wananchi wa…
Sisitizo la kuendelezwa “medani za pamoja za mapambano” na kuangaliwa Israel kama adui wa pamoja wa Wapalestina wote
Huku utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ukiwa umeanzisha vita vikali vya kisaikolojia katika siku za hivi karibuni kuulenga uhusiano wa Hamas na Jihadul-Islami, viongozi wa harakati hizo mbili za muqawama za Palestina wamesisitiza katika mazungumzo yao kwamba wameungana na wako kitu kimopja katika mapambano yao dhidi ya utawala huo ghasibu. Hivi karibuni, utawala wa…
Iran: Utatuzi wa kadhia ya Palestina ni msingi wa utulivu na usalama
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Bagheri Kani amesema utatuzi wa kadhia ya Palestina ndio msingi wa kuanzishwa utulivu na usalama Asia Magharibi (Mashariki ya Kati), na kueleza kwamba mpango wowote unaopuuza haki za taifa la Palestina husababisha kukosekana utulivu na kuvuruga usalama wa eneo hilo. Bagheri Kani aliyasema hayo katika mkutano…
Undumakuwili wa Marekani kuhusu suala la uhuru wa kujieleza
Kufuatia matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Nader Hashemi, Mhadhiri na Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Mashariki ya Kati katika Chuo Kikuu cha Denver, kuhusiana na uwezekano wa Israel kuhusika katika shambulio dhidi ya Salman Rushdie, Warepublican katika Congress ya Marekani wameonya kuhusu ushawishi wa Iran katika vyuo vikuu vya nchi hiyo na kutangaza kwamba…