Israel yakiri kuwaua watoto Wapalestina Gaza
Utawala wa Kizayuni wa Israel umekiri kuwaua watoto watano Wapalestina katika hujuma yake ya hivi karibuni dhidi ya Ukanda wa Gaza. Utawala huo dhalimu ulianzisha vita dhidi ya Gaza mnamo Agosti 5 na vita hivyo vilimalizika baada ya siku tatu kufuatia upatanishi wa Misri. Jumla ya watu 49 waliuawa shahidi katika hujuma hiyo ya Israel…
Kukiri Mkuu wa Sera za Nje wa EU kwamba Magharibi imeonyesha undumakuwili katika kadhia za Ukraine na Gaza
Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amekiri kuwa nchi za Magharibi zinatumia vipimo vya nyuso mbili na za undumilakuwili kuhusiana na masuala ya kimataifa. Akijibu suali aliloulizwa katika moja ya mahojiano aliyofanyiwa, kuhusu msimamo wa Umoja wa Ulaya kwa watu wa Ukraine na Gaza; pamoja na Borrell kukiri kuwa vimetumika vipimo vya…
Iran: Muqawama wa Kiislamu hauishii tu katika ukanda wa Asia Magharibi
Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, muqawama na mapambano ya Kiislamu si kitu cha kuishia kwenye eneo moja tu. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Ali Bahadori Jahromi alisema hayo jana kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa mnasaba wa tarehe 23 Mordad kwa kalenda ya Kiirani ya…
Kani: Israel inakoseshwa usingizi na kizazi kipya cha Wapalestina
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema kuwaua watoto wa Kipalestina kumegeuka na kuwa jambo la kawaida kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, na umwagaji damu huo unadhihirisha wazi kuwa Wazayuni wanakiogopa kizazi kipya cha Wapalestina. Ali Bagheri Kani alisema hayo jana hapa Tehran katika mazungumzo yake na Mohammed bin Abdulaziz al-Khulaifi,…
Wamagharibi wakosolewa kwa undumakuwili juu ya vita Ukraine na Gaza
Harakati inayopinga dhulma na ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina imekosoa vikali undumakuwili wa nchi za Magharibi kuhusu vita nchini Ukraine kwa upande mmoja na katika Ukanda wa Gaza, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa upande mwingine. Harakati ya Kimataifa ya Kuususia Utawala haramu wa Israel BDS katika taarifa jana Jumamosi…
Nyayo za mafia Waisraeli katika madai ya Wizara ya Sheria ya Marekani dhidi ya IRGC
Wizara ya Sheria ya Marekani imechapisha taarifa inayodai kuwa mtu mmoja kwa jina Shahram Poursafi, ambaye wizara hiyo ilimtaja kuwa mwanachama wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), alipanga kumtumia Mmarekani mmoja kumuua John Bolton na afisa mwingine wa utawala wa Donald Trump. Madhumuni ya njama hiyo imetajwa kuwa ni kulipiza kisasi…
Ghalibaf: Muqawama wa Palestina umetoa bishara ya kuangamia utawala wa Kizayuni
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, muqawama na mapambano ya harakati ya Jihad al Islami ya Palestina mbele ya utawala wa Kizayuni wa Israel yametoa bishara njema ya kuangamia utawala huo pandikizi. Shirika la habari la IRNA limemnkuu Mohammad Bagher Ghalibaf akisema hayo leo katika kikao cha wazi cha Bunge…
Wanamichezo Wairaq wakataa kupambana na timu ya Israel katika mashindano ya Romania
Wanamichezo wawili Wairaqi wa mchezo wa tenisi wamekataa kupambana na wanamichezo kutoka utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika michuano ya Paralampiki inayofanyika nchini Romania. Wanamichezo wengi wanaounga mkono Palestina katika nchi za Kiislamu na Kiarabu hawautambui utawala wa Kizayuni na hawako tayari kupambana na wapinzani wao wanaowakilisha Israel katika mashindano mbalimbali ya michezo. Tovuti…