Jinai ya utawala wa Kizayuni katika kuishambulia Jihad Islami ya Palestina
Ijumaa alasiri, jeshil la utawala wa kigaidi wa Israel lilitekeleza jinai kubwa dhidi ya Wapalestina kupitia mashambulizi yaliyopewa jina la “Operesheni ya Alfajiri”, katika maeneo yanayodhibitiwa na harakati ya Palestina ya Jihad Islami katika Ukanda wa Gaza. Katika jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni, Wapalestina 12 akiwemo mtoto wa miaka 5, pamoja na Taysir al-Jabari,…
Wazayuni: Jihad al Islami imeweka tayari zaidi ya makombora 3000 yakisubiri kufyatuliwa tu
Duru za Kizayuni zimedai kuwa, Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina imeweka tayari kwa ajili ya kufyatuliwa makombora zaidi 3000 baada ya kiongozi wake mmoja kukamatwa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Mapema Jumanne asubuhi, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni waliivamia kambi ya wakimbizi ya Jenin na kumuua shahidi Mpalestina mmoja na kumteka…
Jihad Islami yavurumisha makombora Israel baada ya kamanda wake kuuawa
Harakati ya Jihad Islami ya Palestina imevurumisha makombora zaidi ya 100 katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu zilizopachikwa jina la Israel ikiwa ni katika kulipiza kisasi hatua ya utawala katili wa Israel ya kumuua kamanda wa ngazi za juu wa harakati hiyo. Jihad Islami imesema makombora hayo yaliyovurumishwa usiku wa kuamkia leo ni hatua ya awali…
Raisi alaani ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina Gaza, IRGC yatoa neno
Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel yaliyopelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa makumi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza. Sayyid Ebrahim Raisi amesema hayo leo Jumamosi hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, “Katika jinai zake za jana usiku, utawala wa Kizayuni kwa mara…
Syria yataka mpango wa nyuklia wa Israel uwe chini ya usimamizi wa IAEA
Mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesisitizia ulazima wa vituo vya nyuklia vya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kuwa chini ya ukaguzi na usimamizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA. Bassam al-Sabbagh ameyasema hayo katika hotuba aliyotoa katika mkutano wa kuupitia upya mkataba wa kupiga marufuku uundaji na uenezaji…
Mjukuu wa Mandela: Mapinduzi ya Kiislamu yameipa ilhamu Afrika Kusini
Mjukuu wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amesema Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanatoa ilhamu na motisha kwa taifa hilo la kusini mwa Afrika. Mandla Mandela ambaye yuko Tehran kwa ajili ya kupokea Tuzo ya Haki za Binadamu za Kiislamu amesema hayo katika mazungumzo yake na Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya…
Wazayuni wavamia msikiti wa al Aqsa na kuwatia nguvuni Wapalestina 12
Jeshi la utawala haramu wa Israel limewatia nguvu Wapalestina 12 sambamba na kundi la walowezi wa Kizayuni kuuhujumu msikiti mtukufu wa al Aqsa, ambacho ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu. Msikiti wa al Aqsa ambao ni nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu-Kipalestina katika mji wa Baitul Muqaddas umekuwa ukilengwa na hujuma na hatua za uharibifu za…
Kuwait: Tutaendelea kuisusia Israeli na makampuni yanayoshirikiana nayo
Kuwait imetangaza kuwa itaendelea kuisusia Israel, bidhaa zake na makampuni yanayoshirikiana nayo. Hayo yametangazwa katika Mkutano wa Maafisa wa Ofisi za Kikanda za Kuisusia Israel. Shirika la Habari la Kuwait (KUNA) lilimnukuu mwakilishi wa Kuwait katika mkutano huo, Mashari Al-Jarallah, akisema, “Bidhaa zote ambazo zinashukiwa kuwa za Israeli au za kampuni zilizopigwa marufuku, zinachukuliwa hatua…