
Nasrullah: Maeneo yote ya Israel yapo katika shabaha ya makombora ya Hizbullah
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema makombora yenye usahihi mkubwa katika kulenga shabaha ya harakati hiyo ya muqawama yana uwezo wa kupiga sehemu yoyote ya utawala haramu wa Israel; baharini au ardhini. Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema hayo katika mahojiano na televisheni ya al-Mayadeen yaliyorushwa jana usiku kwa mnasaba…

Waislamu wa Tanzania waadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds na kulaani jina za Israel
Upendo na na hisia ya Waislamu wa Tanzania kwa Palestina huonekana katika mambo kadhaa moja wapo ni hili hapa. Waislamu nchini Tanzania na wapenda amani katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki leo wameungana na wapigania haki duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni…

Jenerali Hajizadeh: Karibuni hivi roketi la kubebea satalaiti la Qaem litakuwa tayari kutumwa angani
Kamanda wa kikosi cha anga za mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema roketi la kubebea satalaiti la Qaem karibuni hivi litakuwa tayari kurushwa kwa ajili ya kutumwa katika anga za mbali. Katika miaka miwili iliyopita, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imejikita katika uundaji maroketi ya kubebea satalaiti na kuweza kupiga hatua…

Baada ya kutimuliwa Russia, shirika la uhajiri wa Mayahudi kuhamishiwa Israel
Sambamba na kushadidi mivutano katika uhusiano wa Russia na Israel, duru za habari zimeripoti kuwa shirika la uhajiri wa Mayahudi limeandaa mpango wa siri wa kuhamishia Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) ofisi yake iliyokuweko mjini Moscow. Gazeti la Jerusalem Post limezinukuu duru za kuaminika zikiripoti kuwa kufuatia uamuzi wa Russia wa kuifunga ofisi ya shirika la…

UN yapitisha azimio dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel
Umoja wa Mataifa umepitisha azimio linalosisitiza kuwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel hauna haki ya kupora rasilimali za watu wa Palestina na za miinuko ya Golan ya Syria unayoikalia kwa mabavu. Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC) limepitisha rasimu ya azimio iliyowasilishwa kwa ushirikiano wa Pakistan,- kwa niaba ya kundi…

Wapalestina 21 wauawa, kujeruhiwa na askari wa Israel Ukingo wa Magharibi
Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limewaua shahidi Wapalestina wawili na kujeruhi wengine 19 katika miji ya Nablus na Jenin katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu. Kwa mujibu wa shirika la habari la Ma’an la Palestina, Wapalestina hao wameuawa na kujeruhiwa mapema leo baada ya wanajeshi makatili wa…

Nasrallah: Hizbullah ilikataa hongo ya Marekani kusitisha makabiliano na Israel
Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon anasema harakati hiyo ilikataa mapendekezo kadhaa ya hongo ya kifedha ya Marekani ili kusitisha mapambano yake na utawala wa Kizayuni wa Israel . Katika mahojiano ya aina yake yaliyorekodiwa miaka 20 iliyopita na kurushwa hewani wiki hii, Katibu Mkuu wa Hezbollah Sayyed Nasrallah anasema harakati hiyo ya mapambano…

Mfalme wa Bahrain amuuzulu waziri wake kwa kukataa kumpa mkono balozi wa Israel
Mfalme wa Bahrain amemuuzulu waziri mwanamke wa nchi hiyo kwa kukataa kumpa mkono balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa mjini Manama na kwa kupinga hatua ya kuanzisha ya uhusiano wa kawaida na utawala huo haramu. Tovuti ya habari ya Shahab News imeripoti kuwa, hivi karibuni ilifanyika hafla katika makazi ya balozi wa Marekani…