Idadi kubwa ya Wapalestina yatiwa nguvuni na jeshi la Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan
Vikosi vya Kizayuni vinavyoikalia kwa mabavu vilianza oparesheni ya kuvamia, kusaka na kukamata Wapalestina katika maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu kuanzia alfajiri ya leo (Jumatatu). Wanajeshi wa utawala ghasibu wa Kizayuni waliwatia mbaroni ndugu wanne waliojulikana kwa majina Muhammad, Bara, Abdul Rahman na Momin Qarawi kutoka kambi ya…
Bolton: Tumekaa kimya katika kipindi ambacho Iran, China na Russia zinaimarisha mahusiano
Mshauri huyo wa zamani wa masuala ya usalama wa Marekani aliionya serikali ya Marekani kwamba kwa sasa mazingatio yetu yapo katika kuimarika kwa uhusiano kati ya Iran, China na Urusi. John Bolton, mshauri wa zamani wa usalama wa taifa wa Marekani, aliionya serikali ya Marekani kwamba anatazama tu kupanuka kwa uwezo wa China duniani na…
Makubaliano kati ya Tehran na Riyadh yapunguza mipango yakikhabithi ya Tel Aviv na chuki ya Amerika dhidi ya Iran
Wataalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati wanaamini kuwa, kuhuishwa uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia kumelifikisha eneo hili katika sura mpya ya kimataifa, ambayo imesababisha kudorora kwa mahesabu ya Washington na kufeli kwa mipango ya Wazayuni na Wamarekani. Watafiti wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa kwa kuunga mkono makubaliano kati ya Iran na…
Raia wa Italia akataa kumfanyia Netanyahu kazi ya ukalimani
Mkalimani wa Kitaliano amekataa katakata kumfanyia kazi ya tarjumu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, na kumtaja mwanasiasa huyo kama mtu hatari. Olga Dalia Padoa awali alikubali ombi la kazi hiyo ya ukalimani alipoombwa na ubalozi wa Israel mjini Rome, lakini baadaye akasema kuwa ameghairi msimamo wake, na hatamfanyia ukalimani Benjamin Netanyahu ambaye…
Shambulio la uwanja wa ndege wa Aleppo; Mashambulizi kwenye njia kuu ya misaada ya kibinadamu
Habari : Utawala wa kibaguzi wa Kizayuni ulilenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aleppo kutoka upande wa Bahari ya Mediterania magharibi mwa Latakia kwa shambulio la kinyama la anga, shambulio lililosababisha uharibifu wa mali katika uwanja huo wa ndege na kuufanya kutotumika tena. Ni wazi kabisa kuwa uvamizi wa kibaguzi wa Israel ulianza kutoka…
Hamas: Jinai za utawala wa Kizayuni hazitawatia hofu watu wa Wapalestina
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa taarifa ikiilaani jinai za Wazayuni huko Jenin na kusisitiza kuwa: Jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na mauaji yake dhidi ya raia wa Palestina kamwe hazitalitia hofu taifa hilo. Ni baada ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kushambulia mji wa Jenin katika Ukingo wa…
Madai ya Utawala wa Mtandao wa Kizayuni: Iran imepanga shambulio la mtandao kwenye Kituo cha Teknolojia cha Technion
Utawala wa Mtandao wa Utawala wa Kizayuni ulidai kuwa shambulio la kimtandao kwenye seva za taasisi ya teknolojia ya utawala huu liliandaliwa na Iran mwezi uliopita. Kwa mujibu wa tovuti ya gazeti la Kizayuni la Ha’aretz, kwa mujibu wa utawala wa mtandao wa Israel, Iran ilipanga mashambulizi ya mwezi uliopita kwenye seva za Technion (Taasisi…
Waislamu watakiwa kususia tende za Israel mwezi wa Ramadhani
Kampeni mpya ya kususia utawala wa Kizayuni imezinduliwa ili kuwataka Waislamu barani Ulaya na maeneo mengine duniani kuangalia lebo za matunda hasa tende na kuepuka kununua tende za utawala haramu wa Israel katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Waislamu wanapaswa kuhakikisha kuwa hawafuturu kwa bidhaa za “ubaguzi wa rangi,” waandaaji wa kampeni hiyo wamesema. “Kwa kuchagua…