Palestina; Bingwa wa mapema wa kombe la dunia la kandanda
Vyombo vya habari vya Qatar vimeitaja Palestina kuwa “mshindi wa mapema” wa Kombe la Dunia. Palestina; “ingawaje Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar bado linaendelea, lakini tayari mshindi wa mapema ashapatikana” . Nchi hii imeiba mioyo na akili za mashabiki wa kandanda duniani.” Haya ni maelezo ya Dima Khatib, mkurugenzi mtendaji wa Al Jazeera…
Xi Jinping: China itaendelea kuunga mkono juhudi za Wapalestina
Rais Xi Jinping wa China amesema serikali ya Beijing inaunga mkono jitihada za taifa la Palestina zinazolenga kuhuisha haki za msingi za Wapalestina. Xi Jingping amesema hayo katika mazungumzo yake na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas huko Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia, pambizoni mwa Kongamano la Kwanza la China na…
Serikali ya Jordan yaionya Israel kuhusiana na hujuma jinai zake dhidi ya Wapalestina
Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Jordan imeuonya utawala haramu wa Israel kuhusiana na kuendelea hujuma na mashambulio dhidi ya miji mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Jordan iliyotolewa leo imetoa mwito wa kukomeshwa uvamizi unaofanywa na utawala ghasibu wa Isarel dhidi…
Azimio la UN: Israel iachane na silaha za nyuklia, ijiunge na NPT
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeunga mkono kwa wingi mkubwa mno wa kura azimio la kuutaka utawala haramu wa Kizayuni wa Israel uachane na silaha zake za nyuklia na kujiunga na Mkataba wa Kuzuia Uundaji na Uenezaji Silaha za Nyuklia (NPT). Katika mkutano wa Baraza Kuu la UN, nchi 149 wanachama wa Umoja wa Mataifa…
Ripoti ya Gazeti la New York Times kuhusu mvutano wa Tel Aviv kwenye mipaka ya ardhi ya Lebanon
Gazeti moja la Marekani liliripoti kuhusu hali tete katika mipaka ya ardhi ya Lebanon na Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kuendelea vitendo vya kichochezi vya jeshi la Kizayuni katika mipaka hiyo na kuwateka nyara wachungaji wa Lebanon kwa tuhuma za ujasusi wa Hizbullah. Gazeti moja la Marekani lilichapisha ripoti kuhusu hatua za jeshi la Kizayuni…
Maandamano ya Wamorocco kupinga uhusiano na Israel
Watu wamefanya maandamano katika maeneo tofauti ya Morocco ili kutoa maoni yao ya kupinga kuhalalisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel. Washiriki wa maandamano hayo yaliyoandaliwa katika miji tofauti kama vile mji mkuu Rabat, walibeba bendera za Palestina na kupiga nara dhidi ya uhusiano wa karibu na utawala wa Tel Aviv. Walitoa wito kwa…
Khiyana zingine mbili za Imarati dhidi ya Palestina
Isaac Herzog, Rais wa utawala haramu wa Israel Jumatatu alasiri aliwali Abu Dhabi mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarat) ikiwa ni safari yake ya pili katika nchi hiyo kwa mwaka huu wa 2022. Herzog pamoja na mambo mengine amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Imarati Mohmammad bin Zayed al-Nahyan. Rais wa…
Ya’alon : Baraza la mawaziri la Netanyahu ni baraza la mawaziri mtenda jinai
Waziri wa zamani wa ulinzi wa Israel ameashiria baraza la mawaziri linaloundwa na Benjamin Netanyahu na kusisitiza kuwa linaonekama kuwa ni baraza la vita. Waziri wa zamani wa vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel, Moshe Ya’alon, amesisitiza kwamba Israel iko katika hali ya mparaganyiko na utata. Ya’alon ameongeza kuwa waziri ajaye wa usalama wa…